Na Amir Zia
Raia wengi wa Pakistan wanasubiri kwa hamu kwa tangazo la uongozi wa Trump kuhusu orodha mpya ya marufuku ya usafiri ambayo huenda ikajumuisha au isijumuishe miongoni mwa raia ambao hawatotakiwa kuingia Marekani.
Hakuna taarifa rasmi kuhusu hilo, lakini taarifa ya shirika la habari la Reuters,ya tarehe 5 Machi, ilinukuu vyanzo vitatu bila kuvitaja vikisema kuwa pamoja na Afghanistan, Pakistan “pia” itakuwa miongoni mwa nchi itakayopendekezwa kwenye orodha ya marufuku ya kusafiri, lakini majina yao hayakufahamika.
Taarifa hiyo iliwashtua sana Pakistan, hasa serikali yake, tabaka la utawala, na raia wenye uwezo kifedha. Ukweli ni kuwa, Pakistan inafahamika kwa kufanya kazi kwa karibu na Marekani, na watu wake wa tabaka la juu ambao wanaongea kiingereza huwa wanaunga mkono mataifa ya magharibi.
Kwenda Marekani kwa ajili ya masomo, kazi, kuanzisha biashara, kuwekeza katika mali na baadaye kuishi huko, hilo bado ni ndoto ya kila mtu aliyepata elimu,msomi na raia wa Pakistani wenye uwezo kwa kuwa Marekani haiwapigi marufuku Pakistani moja kwa moja. Licha ya kuwepo kwa mivutano katika uhusiano, taasisi za usalama za mataifa hayo mawili huwa zinaendelea kushirikiana.
Taarifa ya marufuku ya kusafiri pia iliwashtua zaidi Pakistan, hasa kwa kuwa siku moja kabla ya hapo, katika hotuba yake ya kwanza kwa bunge la Congress,tarehe 4 Machi, Rais Donald Trump alipongeza Pakistan kwa kumkamata kiongozi wa kundi la kigaidi la Daesh-K.
Kwa usaidizi wa shirika la kijasusi la Marekani CIA, mamlaka za Pakistan zilimfuatilia na kumkamata Mohammed Sharifullah maarufu Jafar kutoka mkoa wa kusini magharibi wa Balochistan karibu na mpaka wa Afghanistan na kumkabidhi kwa Marekani.
Miongoni mwa wengine wengi, Jafar pia anashutumiwa kwa kupanga mashambulizi ya kikatili ya kigaidi katika uwanja wa ndege wa Kabul tarehe 26 Agosti, 2021 lililowaua wanajeshi 13 wa Marekani na raia 170 wa Afghanistan.
Asante ya Trump
Serikali ya Shehbaz Sharif ilikuwa bado inafurahia kuhusu “asante ya Trump” na bado kutofikiria kuwa wanaweza kujumuishwa kwenye orodha ya marufuku ya kusafiri.
Lakini kulingana na mabalozi wawili wa zamani wa Pakistan, hakuna haja ya kufurahia sana kuhusu ujumbe wa asante wa Trump. Taarifa hiyo ya Reuters pia lazima ichukuliwe kwa tahadhari sana, walisema.
“Sina taarifa zozote za uhakika kuhusu hili (marufuku ya kusafiri), isipokuwa hizo taarifa za Reuters tu,” Sherry Rehman, balozi wa zamani wa Pakistan nchini Marekani,amemwambia mwandishi huyu. “Sidhani kama hili linawezekana. Itakuwa jambo la kushangaza kama hili litatokea… kwa maoni yangu haitakuwa marufuku ya moja kwa moja kwa Pakistan.”
Masood Khan, balozi mwingine mwandamizi wa zamani wa Pakistan nchini Marekani, alisema kuwa baada ya kusoma taarifa ya Reuters, aliomba kuomba hili lisitokee. “Utakuwa uamuzi mbaya sana na utakuwa na matokeo mabaya zaidi.”
Uhusiano wa Pakistan na Marekani ni muhimu sana. Marekani siyo tu inaagiza kwa wingi bidhaa za Pakistan lakini inaunga mkono shughuli muhimu kati ya Pakistan na mashirika ya fedha duniani kama vile IMF na Benki ya Dunia. Mradi wa sasa wa IMF nchini Pakistan usingewezekana bila uungwaji mkono wa Marekani.
Pamoja na hayo, Uhusiano wa Pakistan na Marekani una historia ya kubadilika kutoka hali moja hadi nyingine.
Pakistan iliungana na Marekani wakati wa kipindi cha vita baridi na kupinga uvamizi wa Sovieti nchini Afghanistan alafu pia wakaungana na Marekani katika vita viilivyojulikana kama vita dhidi ya ugaidi katika nchi hiyo isiyo na bandari kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya 9/11 katika ardhi ya Marekani.
Kufuatia kuondoka kwa vikosi vya NATO vilivyokuwa vikiongozwa na Marekani nchini Afghanistan Agosti 2021, Pakistan ikawa haioni Marekani kama yenye umuhimu.
Mtazamo tofauti kwa Pakistan
Muhula wote wa Rais Joe Biden, uhusiano kati ya mataifa haya mawili bado hauko sawa licha ya kushirikiana katika baadhi ya masuala ikiwemo Pakistan kusaidia wakati wa kujiondoa kwa wanajeshi wa NATO walioongozwa na Marekani kutoka Afghanistan.
Hata hivyo,kufikia mwisho wa muhula, serikali ya Biden iliwekea vikwazo kampuni tatu za kutoka Pakistan, ikiwemo shirika la umma, kwa kusaidia katika mradi wa kutengeneza makombora.
Jambo lilowashangaza Pakistan, ni pale Marekani ilipotangaza kuwa mradi wa makombora ya masafa marefu ni tishio kwa Marekani, ingawa maandalizi yote ya ulinzi ya Pakistan yanaelekezwa kwa adui mmoja tu: India.
Na ndiyo sababu ya ujumbe wa “asante” kutoka kwa Rais Trump ulikuwa na maana sana kwa serikali ya Shehbaz.
Sababu ya pili kwa serikali ya Shehbaz kuonesha kufurahishwa na hatua ya trump ni zaidia kuhusu siasa za nyumbani.
Serikali ya Shehbaz inakabiliwa na upinzani kutoka kwa raia wenye uraia pacha wa Pakistan na Marekani na walio na ushawishi mkubwa ambao wamekasirishwa na kufungwa jela kwa Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan, ambaye bado ni maarufu katika siasa za Pakistan.
Raia wa Pakistan wanaomuunga mkono Imran Khan, walio ndani na nje ya nchi, wanatarajia kuwa Trump atatumia nafasi yake kusaidia aachiliwe huru na wamekuwa wakipigania hili.
Hata hivyo, changamoto ya Pakistan kuendeleza uhusiano mzuri na Marekani ni kubwa zaidi na inavyoangaliwa kwa mtazamo wa asante au hata kama jina la Pakistan halitokuwepo kwenye orodha ya nchi zilizopigwa marufuku ya kusafiri nchini Marekani.
Kuna masuala mengi amayo nchi hizi yanayotofautiana kuhusu kuliko wanayokubaliana nayo. Mabalozi wa Pakistan wanakiri kuwa maeneo ambayo nchi hizi mbili wanakubaliana ni kidogo zaidi kufuatia kuondolewa kwa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan.
Mbali za changamoto za zamani kati ya nchi hizi mbili, ikiwemo hofu ya Marekani kuhusu makombora ya Pakistan na mradi wa nyuklia, ushirikiano wake wa karibu wa kimkakati na China, na matatizo ya Pakistan na mahasimu wao India, ambao sasa ni washirika wa kimkakati wa Marekani, kipindi cha Trump kinaweza kuwashtua Pakistan.
Chini ya uongozi wa rais Trump, Pakistan inaweza kujikuta ikilemewa zaidi kwa sababu ya mfumo wake kidiplomasia usiokuwa wa kawaida au mfumo mpya ambao Marekani utahitaji kuangalia kwa makini.Kwa sasa, Pakistan inaweza kuwa haina umuhimu kwa Marekani, lakini hili linaweza kubadilika wakati wowote kama rais wa Marekani anaweza kuamua kuangazia Pakistan mahsusi au Kusini mwa Asia kwa ujumla,wakati wowote.
Kwa hiyo, muhula wa Trump huenda ukatikisa diplomasia ya Pakistan.
Wanaounga mkono India, wanaopinga Pakistan
Suala ambalo litazidisha changamoto kwa Pakistan na Marekani ni wakati serikali ya Trump ambayo inajumuisha wanaounga mkono India na wenye asili ya India katika ngazi za juu. Baadhi ya viongozi hawa wanaonesha wazi uhasama dhidi ya Pakistan na washirika wake, China.
Kwa mfano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, Mshauri wa masuala ya usalama Mike Waltz na Mkurugenzi wa idara ya ujasusi ya CIA John Ratcliffe – wote wanapinga China. Pakistan huenda ikikabiliwa na shinikizo zaidi kutoka Marekani kuhusu ushirikiano wake na China hasa katika suala la diplomasia.
Katika siku za nyuma, wakati Rubio alipopendekeza muswada dhidi ya Pakistan na unaounga mkono India katika bunge la Seneti, Waltz - mwanajeshi mstaafu- alishinikiza Pakistan kukabiliana na ugaidi ulioaminika kuvuka mipaka – msimamo unaoendana na India.
Miongoni mwa kauli zake za kwanza Ratcliffe akiwa mkurugenzi CIA ilikuwa ni kuwawekea shinikizo Pakistan hatua iliyosababisha kukamatwa kwa Sharifullah.
Tulsi Gabbard, mkurugenzi wa usalama wa taifa shirika linalosimamia idara 18 za ujasusi, ni wa kwanza mwenye asili ya Kihindu kuhudumu katika nafasi hiyo na anaonekana kama anayependelea India zaidi, na ana ushirikiano wa karibu na Wahindu wenye itikadi kali. Mama yake Gabbard aliyezaliwa Indiana alibadilisha dini na kujiunga na Wahindu na kuwapa watoto wake majina ya Kihindu.
Gabbard amekuwa akikosoa Pakistan wakati wa makabiliano ya kijeshi na India 2019.
Alafu, kuna wenye uraia Pacha wa Marekani na India ambao wana nyadhifa muhimu katika serikali ya Trump – kuanzia kwa Kash Petal mkurugenzi wa shirika la makosa ya jinai FBI hadi kwa Ricky Gill ambaye ni mkurugenzi mwandamizi wa Kanda ya Asia Kusini na Kati katika Baraza la Usalama. Pia inajumuisha Kush Desai, Naibu msemaji wa Ikulu, na Saurab Sharma ambaye yuko katika Ofisi ya Rais, kuonesha kuwa wahindi milioni 4.5 walio diaspora wamewakilishwa vyema ndani ya serikali ya Trump.
Kuwepo kwa idadi hii ya raia pacha wa India na Marekani katika ngazi za juu za utawala wa Marekani ni changamoto mpya kwa Pakistan katika uhusiano wao na Marekani.
Namna gani Pakistan, ambayo ushawishi wake unapungua na kuzidi kwa vizingiti dhidi yao, inaweza kusikika nchini Marekani.
Kwa hili, pengine serikali ya Shehbaz inahitaji kushirikiana na raia wa Pakistan walioko diaspora katika mataifa ya magharibi na kuleta utulivu wa kisiasa nyumbani ili waweze kutetea taifa lao katika medani ya dunia.