26 Aprili 2025
Kikijulikana kama Swiss Guard, hiki ni kikosi cha wanaume 135 ambao wana jukumu la kumlinda Papa, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani.
Kikosi cha Swiss Guard kilichoanzishwa mwaka 1506 na Papa Julius wa Pili, kuhakikisha Papa anakuwa salama akiwepo Vatican, na pia kinatoa ulinzi kwa Jumuiko la Makardinali au ‘Papal Conclave’, wakati wa mchakato wa kumchagua Papa mpya.
Askari wa Swiss Guard huchaguliwa kutoka kwa raia wa Uswisi ambao ni Wakatoliki na wawe hawajaoa.