AFRIKA
2 dk kusoma
Baraza la Usalama la UN limelaani mashambulizi ya RSF dhidi ya wakimbizi huko Sudan
Baraza la Usalama la Umoja Wa Mataifa limetoa wito wa kuwajibishwa kwa kikosi cha RSF, kwa mashumbulizi dhidi ya raia.
Baraza la Usalama la UN limelaani mashambulizi ya RSF dhidi ya wakimbizi huko Sudan
Vita kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha RSF vinaendelea El Fasher, Darfur, Sudam / Reuters
18 Aprili 2025

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi ya kikosi cha RSF huko El Fasher na mashambulizi dhidi ya wakimbizi wa ndani katika kambi ya Zam Zam na Abu Shouk huko Sudan, yaliosababisha vifo vya takriban raia 400.

"Wajumbe wa Baraza la Usalama wamelaani vikali mashambulizi ya mara kwa mara ya kikundi cha RSF dhidi ya El Fasher na vile vile katika kambi za wakimbizi wa ndani Zamzam na Abu Shouk katika siku za hivi karibuni," Jerome Bonnafont, Mwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza la Usalama, alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo pia ilisisitiza matakwa ya Baraza ya kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano hayo, huku wajumbe wakitaka kusitishwa kwa mapigano El Fasher na maeneo yaliyoko karibu.

Wito wa kuwalinda raia

"Wajumbe wa baraza walitoa wito kwa wahusika katika mzozo kuwalinda raia na kuzingatia wajibu wao chini ya sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na sheria za kimataifa za kibinadamu," Bonnafont alisema.

Wakati mzozo huo ukiadhimisha miaka miwili, Baraza hilo pia lilisisitiza haja ya mazungumzo ya kisiasa na usitishaji vita endelevu.

"Walihimiza pande zote kushiriki, kwa nia njema, katika mazungumzo ya kisiasa kuelekea usitishaji vita wa kudumu na mchakato wa kisiasa unaomilikiwa na Sudan," aliongeza.

Tangu Aprili 15, 2023, RSF imekuwa ikipambana na jeshi la Sudan kudhibiti nchi, na kusababisha maelfu ya vifo na moja ya machafuko mabaya zaidi ya kibinadamu duniani.

Zaidi ya watu 20,000 wameuawa na milioni 15 wamekimbia makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa na mamlaka za mitaa.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us