Watu wanne wamejikuta matatani baada ya kujaribu kutorosha wadudu aina ya siafu kupitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).
Raia wa Vietnam, Duh Hung na Mkenya Dennis Ng’ang’a walifikishwa mbele ya Hakimu Mwandamizi Njeri Thuku wa JKIA, baada ya kukamatwa wakiwa na jumla ya siafu 300 waliohifadhiwa kwenye vichupa vidogo 140.
Hatua hiyo inakuja muda mfupi baada ya kukamatwa kwa raia wawili wa Ubelgiji ambao walifikishwa kwenye mahakama hiyo hiyo kwa kujaribu kutorosha ‘malkia siafu’ 5,000 waliofichwa kwenye vichupa vidogo 2,244.
Kulingana na Shirika la Huduma za Wanyapori nchini Kenya (KWS), siafu hao wana asili ya Kenya.
Kulingana na KWS, siafu hao waliwekwa kwenye vichupa hivyo ili waweze kuishi kwa kwa miezi miwili na pia wasiweze kugundulika kwa urahisi na mashine maalumu za upekuzi ndani ya uwanja wa JKIA.