AFRIKA
2 DK KUSOMA
Kenya yalenga kutoza ushuru zaidi  katika simu
Mamlaka ya Ushuru Kenya inalenga kupata ushuru zaidi kutoka katika simu zinazoingia nchini ikiwa imedhamiria kukuza msingi wa walipakodi kutoka kwa walipakodi milioni 4 hadi milioni 13 ifikapo 2028/29.
Kenya yalenga kutoza ushuru zaidi  katika simu
Masharti mapya yanayplenga ushuru kutoka kwa simu za rununu yataanza kufanya kazi Januari 2025 / Picha: AA
5 Novemba 2024

Mamlaka ya Ushuru kenya , yaani Kenya Revenue Authority, KRA imetanganza masharti mapya yanayolenga kutoza ushuru simu zinazoingizwa nchini Kenya.

"Waagizaji wote wanatakiwa kuwasilisha maelezo ya kina yanayojumuisha kiasi sahihi, maelezo ya kina ya modeli, na nambari husika za Utambulisho wa Kimataifa wa Kifaa cha Simu (IMEI) kwa kila kifaa cha rununu," KRA imesema katika taarifa yake kwa umma.

KRA imesema wanaohusika katika utengenezaji wa vifaa lazima wajisajili kwenye tovuti ya Forodha ya KRA na wawasilishe ripoti ya vifaa vyote vilivyokusanywa kwa ajili ya soko la ndani, pamoja na nambari zao za IMEI.

"Abiria wanaoingia nchini Kenya pia watahitajika kutangaza vifaa vyao vya rununu kwenye fomu ya tamko la abiria F88, kutoa maelezo muhimu ya nambari za IMEI kwa vifaa vinavyokusudiwa kutumiwa wakati wa kukaa," KRA imeongezea.

Masharti haya mapya yataanza kufanya kazi Januari 2025.

KRA inatarajiwa kukusanya Kshs. trilioni 20.486 ( zadi ya bilioni $158) katika kipindi cha miaka mitano ijayo, kulingana na Malengo ya Bajeti .

Ili kufanikisha hili, KRA imedhamiria kukuza msingi wa walipakodi kwa walipakodi milioni 4 hadi milioni 13 ifikapo 2028/29.

Notisi rasmi ya KRA inajiri wiki moja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya kutangaza kuwa simu za rununu ambazo hazitimizi sheria mpya za ushuru hazitahusishwa na huduma ya kampuni yoyote ya simu nchini.

Katika taarifa, serikali iliamuru kuwa watoa huduma za mtandao wa simu waunganishe vifaa kwenye mitandao yao baada ya kukagua hali yao ya kufuata kodi kwa kutumia hifadhidata ya orodha iliyoidhinishwa ya vifaa vinavyotii sheria.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us