ULIMWENGU
4 dk kusoma
Operesheni ya Spiderweb: Gharama ya kutoenda na wakati kuhusu mbinu za kivita
Inafahamika kama mbinu mbaya ya kisasa, Operesheni Spiderweb ya Ukraine inafanya kuwe na ulazima wa kubadilisha mbinu za kisasa za vita.
Operesheni ya Spiderweb: Gharama ya kutoenda na wakati kuhusu mbinu za kivita
PICHA YA MAKTABA: Picha za Satelaiti zikionesha ndege zilizoharibiwa na barabara katika uwanja wa kijeshi wa Belaya, Urusi. / Reuters
10 Julai 2025

Kwa muda mrefu udanganyifu na ujasusi umetumika kama mbinu za kivita, tangu zamani za kale. Katika mapigano ya kisasa mbinu kama hizo zimeanza kurejea tena kama inavyoonekana katika mbinu na operesheni thabiti za kijasusi. Mifano ya hivi punde inaonesha namna gani teknolojia ya kisasa inavyofanya kazi, kutoka kwa ndege zisizo na rubani hadi kwenye vilipuzi. 

Wakati ndege kadhaa zisizo na rubani ziliposhambulia ndani ya Urusi ikiwa sehemu ya Operesheni Spiderweb ya Ukraine, Juni 1, na kuharibu mizinga ya kurusha mabomu, ilitoa changamoto kuhusu namna uwezo unavyoangaziwa na kulindwa.  

Mashambulizi hayo yalichangiwa na juhudi za operesheni ya kijasusi. Ndege zisizo na rubani zilizokuwa zimefichwa ndani ya nyumba zilotengenezwa kwa mbao na kusafirishwa kwa kutumia magari zilishambulia viwanja vinne kati ya vitano vya ndege za kijeshi,kuashiria uwezo wa Ukraine wa kufika katika ardhi ya Urusi. Shambulio hilo liliharibu ndege za kijeshi zaidi ya 20 na kuharibu makombora yasiyopungua 12 ya Urusi.

Huku watu wakiangazia mbinu za kivita zinazotumia teknolojia ya hali ya juu, kitu kimoja kilichokuwa wazi katika Operesheni Spiderweb ni kuwa ndege hizo za Ukraine moja inagharimu chini ya dola ya elfu moja. Katika kipindi ambacho serikali zinaongeza matumizi yake katika masuala ya ulinzi, tukio hili ni ukumbusho kuwa matumizi makubwa hayatafsiri kuwa usalama zaidi.

Katika enzi ambazo matumizi ya kijeshi kote duniani yamefika dola trilioni 2.7 mwaka 2024, ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi tangu kumalizika kwa Vita Baridi, kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, matumizi ya teknolojia ya hali ya juu yanashangaza. Nchi tano pekee —Marekani, China, Urusi, Ujerumani na India—zilikuwa na asilimia 60 ya matumizi hayo. Marekani pekee ilitumia karibu dola trilioni 1.

Kuongezeka huku kumesababisha wasiwasi, kupungua kwa imani kuhusu miungano, na hali tete kuhusu mfumo mpya wa kimataifa. Vita vya Urusi nchini Ukraine, Israel kuendelea kushambulia Gaza, wasiwasi kuhusu kutegemea Marekani kama mdhamini wa usalama, na kutumia teknolojia zaidi kumesababisha hali ya wasiwasi. 

Kutokuwepo kwa juhudi mahsusi za kubadilisha vikosi vyao kwa kutumia teknolojia za kisasa, majeshi yako kwenye hatari ya kutumika sana na kushindwa kwenda na wakati.

Kuongezeka kwa bajeti za ulinzi hakuondoi nafasi ya uwazi ya kimkakati.

Kubadilisha mifumo

Mifumo, magari ya kijeshi, ndege za kivita, bado ni muhimu kwa operesheni za kijeshi, hasa kwa kuzuia na kujihusisha na mazungumzo ya ngazi za juu. Lakini bila kujumuisha katika mitandao, mifumo, ambayo inajumuisha ile ambayo haina rubani, Uongozaji unaotumia Akili Mnemba, na kukusanya taarifa za ujasusi, ufuatiliaji, umuhimu wao unaenda ukiisha. 

Mapigano ya hivi karibuni, kutoka kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine hadi katika vurugu za mpakani mwa India na Pakistan, yamedhihirisha matatizo ya kimkakati.

Sasa hivi siyo suala la kubahatisha kuhusu mabadiliko. Tayari yanaonekana katika uwanja wa vita, ambapo kuna silaha nje nje, ndege nyingi zisizokuwa na rubani, na kulenga kwa kutumia Akili Mnemba kunabadilisha mifumo ya kuangazia vita.

Baadhi ya majeshi yanakwenda na wakati. Mkakati wa Uingereza wa “20-40-40”, kwa mfano, unaangazia asilimia 20 itaongozwa na watu, asilimia 40 mifumo itakayotumika bila kuongozwa, na asilimia 40 ya mifumo kama silaha.

Mifumo hii inawezekana kwa kuwezesha ushirikiano kuliko kutegemea uwezo wa sehemu moja, ikilenga mifumo yenye uwezo mkubwa na ile ambayo ni nafuu.

Operesheni Spiderweb: Kutatiza mikakati

Ukraine ilidhihirisha namna mifumo hii inavyofanya kazi. Kufuatia mipango ya miezi 18, Shirika la Ujasusi la Ukraine(SBU) liliingiza ndege zisizokuwa na rubani 117 ndani ya Uturuki, kwa kuzificha ndani ya magari.

Kwa wengi, operesheni hiyo iliwakumbusha tukio la Pearl Harbour, siyo kwa ukubwa wake, lakini kwa uwezo wake wa kuweka historia mpya ya sheria za kivita.

Kwa gharama ndogo ya silaha zao, Ukraine ilifanikiwa kuishambulia Urusi na kuipa hasara ya mabilioni ya madola.

 Enzi za matumizi ya mifumo nafuu

Mafanikio ya Ukraine hayakuwa ya kawaida. Operesheni Spiderweb inaonesha namna gani mifumo ya kisasa ya vita inavyobadilika. Nchi hiyo ilitengeneza ndege zisizokuwa na rubani milioni 2.2 mwaka uliopita na inapanga kuongeza idadi hiyo maradufu.

Katika mazingira ambayo silaha za gharama kubwa zinaweza kuharibiwa na silaha za bei nafuu, viwanja vya ndege vya kijeshi viko hatarini zaidi. Bila kuwepo kwa ubunifu katika itikadi, hata ukiwa na silaha zenye uwezo zaidi hazisaidii chochote.

Hii inaonesha umuhimu wa kuwa na mifumo mingi zaidi ya ulinzi ambayo ni zaidi ya itikadi—uwezo wa kukabiliana na ndege zisizokuwa na rubani, silaha nzito, na mbinu za kisasa na kielektroniki za kivita.

Operesheni Spiderweb imesababisha hali ya shauku miongoni mwa wanachama wa NATO, ambapo matumizi ya pamoja ya Ukraine ya Akili Mnemba katika uwanja wa vita yanafanyiwa utafiti wa karibu. Huku ikiwa na wanajeshi wachache, imeamua kutumia teknolojia zaidi, kufanya mbinu ya ujasusi kuwapa uhakika wa mashambulizi.

Kwa muktadha huu, swali la msingi kwa wanaofanya mipango ya ulinzi siyo kuhusu kiasi gani wanachotaka kutumia. Uwekezaji wa ulinzi kwa mustakabali wao utakwenda sanjari na vitisho vilivyopo sasa, au matukio yaliyokuwepo kabla ya wakati huu?

CHANZO:TRT Global
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us