AFRIKA
2 dk kusoma
Rwanda yaruhusu raia wake walio ughaibuni kufanya miamala ya mali bila kurudi nyumbani
Serikali ya Rwanda imeidhinisha ruhusa kwa raia wake walio ughaibuni kufanya miamala ihusuyo mali zao bila kurudi nchini mwao.
Rwanda yaruhusu raia wake walio ughaibuni kufanya miamala ya mali bila kurudi nyumbani
Mfumo wa kidijitali wa Rwanda / picha: @IremboGov / Public domain
10 Julai 2025

Raia wa Rwanda wanaoishi ng'ambo sasa wataweza kutumia mchakato rahisi wa kutoa nguvu ya uwakilishi kufanya miamala inayohusiana na mali zao pasipo kulazimika kurudi nchini mwao.

Kwa sasa, baadhi ya wanyarwanda, wanalazimika kusafiri umbali hadi kwenye balozi zao huko ughaibuni, ili waweze kuidhinishiwa uwakilishi wa uhamishaji mali, licha ya kuwepo kwa mifumo ya kidijitali.

Hatua hii, inalenga kurahisisha na kufanikisha usimamizi wa Maendeleo yanalenga kufanya usimamizi wa ardhi kuwa wa ufanisi zaidi.

"Kwa sasa, haitokuwa lazima kwa mtu kupanda ndegena ili kwenda kutafuta hati ya uwakilishi wa uhamishaji mali kutoka ubalozini," alisema Sylvain Muyombano, Mkuu wa Idara ya Utawala wa Ardhi kutoka Mamlaka ya Ardhi nchini Rwanda (NLA).

Hapo awali, Wanyarwanda wanaoishi ng'ambo walitakiwa kuwasilisha moja kwa moja hati halisi kwa balozi za Rwanda ili kutoa mamlaka ya kisheria kwa wawakilishi wao nchini kwa ajili ya kuhamisha mali.

Hata hivyo, huduma hii sasa inaweza kupatikana kwa njia ya kidijitali kupitia tovuti ya serikali ya IremboGov, chini ya huduma zinazosimamiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (MINAFFET).

Huduma hiyo inaruhusu Wanyarwanda au raia wa kigeni wanaoishi ng'ambo kuidhinisha kisheria mtu anayeaminika nchini Rwanda kuchukua hatua kwa niaba yao katika masuala yanayohusu mali inayohamishika na isiyohamishika.

Mali hizo ni pamoja na ardhi, nyumba, magari, hisa za kampuni na mali nyingine muhimu.

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us