UTURUKI
1 dk kusoma
Erdogan amuambia Stocker: Fursa ya kumaliza vita vya Urusi na Ukraine haipaswi kupotezwa
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anajadili uhusiano wa mataifa mawili, pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa, na Kansela wa Austria Christian Stocker.
Erdogan amuambia Stocker: Fursa ya kumaliza vita vya Urusi na Ukraine haipaswi kupotezwa
Erdogan alisisitiza kwamba kufikisha misaada ya dharura ya kibinadamu huko Gaza haraka iwezekanavyo ni jambo la muhimu sana. / AA
10 Julai 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa fursa ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine haipaswi kupotezwa.

Erdogan amejadili uhusiano baina ya mataifa mawili, pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa na Kansela wa Austria Christian Stocker kupitia mazungumzo ya simu, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki ilisema Alhamisi.

Katika mazungumzo hayo, Erdogan alisisitiza kwamba kufikisha misaada ya dharura ya kibinadamu huko Gaza haraka iwezekanavyo ni muhimu.

Kuhusu Syria, alisema kuwa Uturuki inaendelea na juhudi zake za kuhakikisha utulivu nchini humo na kwamba kuongeza ustawi wa kijamii na kiuchumi ni muhimu ili kuwezesha kurejea kwa wakimbizi wa Syria katika nchi yao.

Rais Erdogan alisema Uturuki na Austria zinapaswa kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika sekta ya biashara na uwekezaji na kwamba wataendelea kuchukua hatua za kuimarisha ushirikiano.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us