AFRIKA
2 dk kusoma
Raia wasiopungua 62 wameuawa kutokana mashambulizi ya RSF katika eneo la Darfur, Sudan
Wananawake 17, na watoto 15 ni miongoni mwa waliouawa, jeshi limesema
Raia wasiopungua 62 wameuawa kutokana mashambulizi ya RSF katika eneo la Darfur, Sudan
17 Aprili 2025

Raia wa Sudan wasiopungua 62 wameuawa, na wengine 75 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya vikosi vya RSF huko El-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini magharibi mwa Sudan, jeshi lilisema siku ya Alhamisi.

Taarifa kutoka kwa jeshi inasema kuwa wanawake 17 na watoto 15 ni miongoni mwa waliouawa katika mashambulizi yaliyolenga mji huo siku ya Jumatano.

Jeshi linasema maafisa wake walikabiliana na mashambulizi ya RSF katika mji huo, na kuwaua wapiganaji 70, pamoja na kuwajeruhi wengine kadhaa, na kuharibu magari yao ya vita 15 na malori mawili ya mafuta.

Hakukuwa na taarifa ya haraka kutoka kwa waasi hao kujibu yaliyosemwa na jeshi.

Kumekuwa na makabiliano makali katika eneo la El-Fasher kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF tangu Mei 2024, licha ya jumuiya ya kimataifa kuonya kuhusu kupigana katika mji huo, ambao ni muhimu kwa shughuli za misaada kwa ajili ya majimbo yote matano ya Darfur.

Mapema wiki hii, kundi la the RSF lilidai kuchukua udhibiti wa kambi ya wakimbizi ya Zamzam huko El-Fasher baada ya kukabiliana na vikosi vya jeshi. Raia wasiopungua 400 waliuawa na karibu 400,000 kuondolewa katika eneo hilo kutokana na mapigano, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Tangu Aprili 15, 2023, wapiganaji wa RSF wamekuwa wakikabiliana na jeshi la Sudan kutaka kuchukua udhibiti wa nchi, na kusababisha mauaji ya maelfu ya watu na moja ya hali mbaya zaidi kwa watu duniani.

Zaidi ya watu 20,000 wameuawa na wengine milioni 15 kulazimika kuondoka katika makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa na serikali za mitaa.

Hata hivvyo, utafiti kutoka kwa wasomi wa Marekani, unakadiria, idadi ya waliouawa kuwa karibu 130,000.

Katika wiki za hivi karibuni, RSF imepoteza maeneo kadhaa kote nchini Sudan baada ya kukabiliwa na vikosi vya serikali.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us