Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imejibu vikali kauli za kichokozi zilizotolewa na mawaziri wa Israeli dhidi ya Uturuki.
Katika taarifa yake iliyotolewa Aprili 3, 2025, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imesema kauli hizo zilikuwa zenye kuakisi utimamu wa akili wa Israeli kwa sasa, pamoja na sera zao kandamizi na za kibaguzi.
Kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, inashangaza kuona kwanini Israeli inakerwa na maendeleo ya Syria na Lebanon, huku yakiungwa mkono na ulimwengu mzima.
Licha ya kutowepo kwa vitisho vyovyote dhidi yake, Israeli bado iliishambulia Syria siku ya Aprili 2, kiashirio cha sera zao zenye kuegemea machafuko.
“Kuilaumu Uturuki hakutoficha mauaji ya Gaza, vita dhidi ya Wapalestina, na mashambulizi ya kanda, nia yao ya kumega eneo la Ukingo wa Magharibi na nia yao ya kujitanua, kupitia kuzishambulia Syria na Lebanon, huku ikiilenga Uturuki,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Tishio la Israeli kwa usalama wa kanda
Wizara hiyo imesisitiza kuwa Israeli inaendelea kuwa tishio kwa usalama wa kanda nzima, kupitia mashambulizi yao yenye kulenga umoja na utawala wa mataifa katika ukanda huo.
“Kwa makusudi kabisa, Israeli inatatiza usalama wa kanda yetu, ikisababisha machafuko na kukuza ugaidi,” ilisema taarifa hiyo.
Kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, ili kuwepo kwa usalama katika eneo lote la kanda, Israeli inapaswa kuachana na sera zake pamoja na kukandamiza jitihada za upatikanaji amani nchini Syria.
“Ni lazima jumuiya ya kimataifa ichukue hatua sasa ili kupunguza udhalimu wa Israeli,” iliongeza.