Mchezaji wa safu ya ulinzi Virgil van Dijk ameongeza muda wa mkataba wake na Liverpool utakaomuweka Anfield hadi 2027, timu hiyo ya Ligi Kuu ya England ilitangaza kwenye mtandao wake.
Van Dijk, 33, alisema: "Nina furaha sana, najisikia fahari. Nina hisia nyingi kwa sasa wakati ninapozungumzia suala hili.”
"Ni jambo la fahari kwa kweli, ni hisia ya furaha. Ni jambo zuri sana. Safari niliyopitia hadi kufikia sasa katika soka, kuweza kuiongeza tena kwa miaka mingine miwili katika klabu hii ni jambo zuri sana na nimefurahi zaidi," aliongeza.
Mchezaji huyo wa safu ya ulinzi mahiri ameisaidia Liverpool kushinda mataji kadhaa, ikiwemo Kombe la Ligi ya mabingwa Ulaya 2018-19, Kombe la UEFA la Super Cup 2019-20 , Kombe la Dunia la FIFA kwa klabu 2020, na taji la Ligi Kuu ya England 2019-20, pamoja na Kombe la FA 2022.