AFRIKA
2 dk kusoma
Rais wa Uganda afanya mazungumzo na viongozi wa Sudan Kusini kujaribu kuepusha vita kulipuka
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini Mohammed Abdallah Goc alisema kuwa uongozi wa nchi hiyo umemhakikishia Museveni kuhusu dhamira yake ya kutekeleza makubaliano ya amani.
Rais wa Uganda afanya mazungumzo na viongozi wa Sudan Kusini kujaribu kuepusha vita kulipuka
Uganda mwezi uliopita ilituma wanajeshi wake Sudan Kusini kuunga mkono serikali, lakini ilikosolewa na chama kikuu cha upinzani cha Sudan Kusini SPLM-IO. / AP
5 Aprili 2025

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alitarajiwa kukutana na maafisa wa Sudan Kusini katika siku ya pili ya safari yake katika mji mkuu, Juba, huku Umoja wa Mataifa ukieleza wasiwasi wake kuhusu kuzuka upya kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kiongozi mkuu wa upinzani kuwekwa katika kifungo cha nyumbani.

Museveni, ambaye ni miongoni mwa wadhamini wa mkataba wa amani wa 2018 uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano, alifanya mazungumzo ya faragha na Rais Salva Kiir siku ya Alhamisi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini Mohammed Abdallah Goc alisema kuwa uongozi wa nchi hiyo umemhakikishia Museveni kuhusu dhamira yake ya kutekeleza makubaliano ya amani.

Hali ya kisiasa ya Sudan Kusini bado ni tete na ghasia za hivi majuzi kati ya wanajeshi wa serikali na makundi yenye silaha wanaoungwa mkono na upinzani zimezidisha hali ya wasiwasi.

Machar yuko kifungo cha nyumbani

Uganda mwezi uliopita ilituma wanajeshi nchini Sudan Kusini kuunga mkono serikali, lakini ilikosolewa na chama kikuu cha upinzani nchini Sudan Kusini SPLM-IO, ambacho kiongozi wake Riek Machar yuko chini ya kifungo cha nyumbani kwa tuhuma za uchochezi.

Mapema mwezi Machi, kundi lenye silaha linalomtii Machar lilishambulia helikopta ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa katika misheni ya kuwaondoa wanajeshi wa serikali kutoka katika Jimbo la Upper Nile la kaskazini mwa nchi hiyo.

Nchi za Magharibi zikiwemo Ujerumani na Norway zimefunga kwa muda balozi zao mjini Juba huku Marekani na U.K zikipunguza wafanyakazi wa ubalozi huo.

CHANZO:AP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us