Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametaka kuwepo kwa jitihada za pamoja za kutambua kimataifa “mauaji ya kimbari’ yanayofanywa nchini mwake.
Tangu mwaka 1996, mgogoro wa mashariki mwa DRC umesababisha vifo vya takriban watu milioni sita, kwa mujibu wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Uhusiano wa Mambo ya Nje.
Akizungumza katika uzinduzi wa Mazungumzo ya Mduara ya Gharama ya Mauaji ya Kimbari siku ya Jumanne, Tshisekedi amesisitiza haja ya “mapambano ya pamoja” ya kutambua mauaji, kwa mujibu wa Wakala wa Habari wa Congo-ACP.
Mazungumzo hayo, yaliyoanzishwa na Jukwaa la Vijana wa Congo (CAYP), yanalenga kuifanya Agosti 2 ya kila mwaka kuwa siku ya maadhimisho ya waathirika wa vita katika katika historia ya DRC.
“Mazungumzo haya hayatakiwi tu kutuwezesha kushuhudia, lakini zaidi, kufanya kazi pamoja ili kujenga mkakati madhubuti wa kitaifa ili kutapa utambulisho wa kimataifa wa mauaji ya kimbari yanayofanywa katika ardhi yetu na kutafuta amani ya kudumu katika nchi yetu,” amesema Rais Tshisekedi.
‘Vikwazo vya kidiplomasia’
Rais Tshisekedi ametambua kuwepo kwa baadhi ya changomoto katika ufuatiliaji huo.
“Wapenda nchi wenzangu, safari yetu ya kutafuta ukweli na amani inakabiliwa na pingamizi za kisiasa, kidiplomasia na vikwazo vya kifikra, lakini ni lazima kutorudi nyuma,” amesema.
Tshisekedi amehimiza jitahada za DRC kuweka siku ya maadhimisho ya mauaji ya kimbari licha ya vikwazo vya kidiplomasia,” na kusema nchi yake itashinda dhidi ya giza na kujenga mustakbali wenye amani, haki na heshima.”