AFRIKA
2 dk kusoma
Hofu kubwa yatanda DRC kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa surua
Kumekuwepo na maambukizi 12,000 na vifo 180 hadi kufikia sasa.
Hofu kubwa yatanda DRC kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa surua
Kulingana na Africa CDC, maeneo yalioathirika zaidi ni pamoja na majimbo ya Kivu kaskazini na Kivu Kusini./Picha: @WHO / Others
3 Aprili 2025

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (Africa CDC) kimeonesha wasiwasi kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa surua ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Kulingana na Africa CDC, maeneo yalioathirika zaidi ni pamoja na maeneo ya Kivu kaskazini na Kivu Kusini.

Hadi kufikia sasa, idadi ya maambukizi imefikia 12,000 huku watu 180 wakipoteza maisha.

"Iwapo viongozi wetu wa kanda watashindwa kutuhakikishia usalama, mimi nitakuwa wa kwanza kusafiri hadi DRC, nikipeleka madawa kwa wale wenye mahitaji zaidi," alisema Jean Kaseya, Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC katika mkutano kwa njia ya mtandao uliofanyika Aprili 3, 2025.

"Tumesikitishwa sana na uwezo wetu wa kupima ugonjwa wa mpox huko Kivu, kwani kutokana na hali ya vita inavyoendelea, tumefanikiwa kupima watu kwa asilimia 18 tu.”

Hali kadhalika, Kaseya alionesha wasiwasi wake kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Sudan Kusini, ambapo hadi sasa, idadi ya maambukizi imefikia milioni moja.

"Suala la chanjo bado linabakia kuwa changamoto huko Sudan Kusini kutokana na hali ya usalama ilivyo," aliongeza.

Kuhusu misaada kutoka nje, Kaseya alisema kuwa alifanikiwa kuonana na washauri wawili wa Rais wa Marekani Donald Trump, ambao wamemuhakikishia kuendelea kutoa  msaada kwenye maeneo nyeti ya sekta ya afya ya umma.

"Sio Marekani tu iliyositisha misaada kwa bara la Afrika hususani katika huduma ya afya, tunazungumzia mataifa 12 ambayo yamepunguza kutoka Dola Bilioni 81 hadi 25,” alisema.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us