MICHEZO
1 dk kusoma
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania apokea salamu maalumu kutoka Manchester United
Rais Samia alipokea salamu hizo kutoka kwa mmiliki wa klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe, jijini Dar es Salaam, Aprili 11, 2025.
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania apokea salamu maalumu kutoka Manchester United
Kwa mujibu wa taarifa ya iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X wa Ikulu ya Tanzania, ujumbe wa klabu hiyo maarufu ulimwenguni, ulifanya mazungumzo na Rais Samia ambapo pia mmiliki wa Manchester United, alielezea dhamira yake ya kuitumia Klabu yake kutangaza utalii nchini Tanzania./Picha: @ikulumawasliano / Others
11 Aprili 2025

Wachezaji na viongozi wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, wakiongozwa na Sir Alex Ferguson na kocha wa sasa wa ‘Mashetani hao Wekundu’, Ruben Amorim, wametuma salamu kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia alipokea salamu hizo kutoka kwa mmiliki wa klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe, jijini Dar es Salaam, Aprili 11, 2025.

Kwa upande wake, mmiliki wa Manchester United, ameeleza dhamira yake ya kuitumia Klabu yake kutangaza utalii nchini Tanzania, huku Rais Samia akimkaribisha kuanzisha vituo vya mafunzo ya michezo, maarufu kama ‘Sports Academies.’

Kwa mujibu wa taarifa ya iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X wa Ikulu ya Tanzania, ujumbe wa klabu hiyo maarufu ulimwenguni, ulifanya mazungumzo na Rais Samia ambapo pia mmiliki wa Manchester United, alielezea dhamira yake ya kuitumia Klabu yake kutangaza utalii nchini Tanzania.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us