AFRIKA
3 dk kusoma
Lesotho yatuma ujumbe nchini Marekani kushughulikia suala la ushuru wa Trump
Nchi ya Afrika Kusini pia imesema itafanya mazungumzo na Marekani kuhusu suala la ushuru uilowekwa hivi karibuni na Trump.
Lesotho yatuma ujumbe nchini Marekani kushughulikia suala la ushuru wa Trump
Viwanda vingi vinahofiwa kuathirika kufuatia ushuru mpya uliowekwa na Rais wa Marekani Donald Trump. / Reuters
4 Aprili 2025

Nchi ya Lesotho imetuma wajumbe wake siku ya Ijumaa kuelekea jijini Washington kujadiliana na Marekani kuhusu ushuru ambao unahatarisha kuathiri karibu nusu ya mauzo yake ya nje, waziri wake wa biashara alisema, katika kile kinachoweza kuwa pigo kubwa la uchumi wake.

Ushuru wa 50% wa biashara uliowekwa dhidi ya nchi hiyo ilioko kusini mwa Afrika ulikuwa wa juu zaidi katika orodha ya nchi zinazolengwa na Rais wa Marekani Donald Trump.

"Mielekeo ya hivi punde ya sera iliyofanywa na Marekani inashangaza ... kwani Marekani imekuwa soko muhimu sana kwa Lesotho," Waziri wa Biashara Mokhethi Shelile aliliambia bunge siku ya Ijumaa, akiongeza kuwa asilimia 45 ya mauzo ya nje ya nchi yalikwenda Marekani.

Alisema kwamba maofisa tayari wameshirikiana na ubalozi wa Marekani "kufafanua ni jinsi gani, kwa nini Lesotho ilijumuishwa katika orodha ya ushuru wa juu kama huo".

Mwezi uliopita, Donald Trump alizua taharuki baada ya kuitaja Lesotho kuwa nchi ''hakuna mtu aliyewahi kusikia.''

Ujumbe wa ngazi ya juu

Trump siku ya Jumatano aligonga washirika wa kibiashara wa Marekani kwa ushuru, ukiondoa miongo kadhaa ya biashara inayozingatia sheria ambayo wanaharakati wamesema kwa muda mrefu inapendelea nchi tajiri kama Marekani.

Mauzo ya Lesotho kwenda Marekani, mengi yakiwa ya nguo za chapa maarufu kama vile Levis, yaliongezeka hadi dola milioni 237 mwaka 2024 na ni zaidi ya sehemu ya kumi ya Pato la Taifa.

"Lesotho itatuma wajumbe wa ngazi ya juu nchini Marekani ili kujaribu kudumisha hali ya sasa ya soko," Shelile alisema.

Aidha nchi hiyo imesema "itaongeza juhudi za kuuza nje kwa masoko mbadala kama vile Umoja wa Ulaya na eneo la biashara huria la Afrika".

Nchi hiyo yenye watu milioni 2 ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, na Pato lake la Taifa kwa kila mtu lilikua $916 mwaka 2023, kulingana na takwimu za Benki ya Dunia.

Afrika Kusini pia imeshtushwa na ushuru wa Trump

Wakati huo huo, serikali ya Afrika Kusini ilisema Ijumaa kwamba ushuru uliotangazwa na Rais Donald Trump wiki hii ulibatilisha vifungu vya mpango wa biashara wa Marekani, Sheria ya Ukuaji na Fursa Afrika (AGOA).

AGOA, ambayo inatoa fursa kwa mataifa ya Afrika kuuza bidhaa zao bila ushuru katika soko la Marekani, inatazamiwa kuisha mwezi Septemba. Huku ushuru uliowekwa na Trump ukitoa dalili wa kutowekwa upya mkataba wa biashara uliopitishwa mwaka 2000.

Wkihutubia mkutano na waandishi wa habari, mawaziri wa mambo ya nje na biashara wa Afrika Kusini walisema serikali inaweza kutafuta misamaha ya ziada na makubaliano ya mgawo na Marekani pamoja na kutafuta masoko mbadala ya nje.

"Hatua kubwa za ushuru zitaathiri sekta kadhaa za uchumi wetu, ikiwa ni pamoja na sekta ya magari, kilimo, chakula, vinywaji vilivyosindikwa, kemikali, metali na sehemu nyingine za viwanda, huku kukiwa na athari kwa ajira na ukuaji," mawaziri hao wawili walisema katika taarifa ya pamoja.

"Serikali itawekeza kimkakati katika viwanda vilivyoathiriwa na ushuru huo, kusaidia ukuaji wa uchumi kupitia uboreshaji wa kisasa na maendeleo ya miundombinu."

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us