AFRIKA
1 dk kusoma
Afrika Kusini yatafuta mikataba mipya ya biashara na Marekani
Shinikizo la Afrika Kusini linakuja baada ya uongozi wa Trump kuziwekea nchi nyingi duniani ushuru mpya wa bidhaa zinazoingizwa nchini humo.
Afrika Kusini yatafuta mikataba mipya ya biashara na Marekani
Uhusiano kati ya Afrika Kusini na Marekani umekuwa wa kutatanisha tangu Trump kuingia madarakani Januari. / TRT Afrika
3 Aprili 2025

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema ushuru mpya uliowekwa na Marekani unaonyesha umuhimu wa kujadiliana makubaliano mapya ya kibiashara na Washington ili kuhakikisha uhakika wa biashara wa muda mrefu.

Kauli hii inakuja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza ushuru mpya kwa bidhaa nyingi zinazoingizwa nchini Marekani Jumatano.

Trump ameweka kiwango cha asilimia 30 kwa Afrika Kusini.

“Ushuru unathibitisha uharaka wa kujadili na Marekani makubaliano mapya ya biashara yenye faida kwa pande zote, kama hatua muhimu ya kuwa na uhakika wa muda mrefu wa biashara,” amesema Rais katika taarifa yake Alhamisi.

Ushuru uliowekwa hivi karibuni ni nyongeza ya asilimia 25 iliyowekwa kwa magari yote na vipuli vinavyoingizwa nchini Marekani, ambao utaanza rasmi Alhamisi.

Uuzaji wa magari na vipuli vya Afrika Kusini nchini Marekani unakadiriwa kufikia zaidi ya dola bilioni 2 na unaweza kuathirika zaidi na ushuru mpya.

“Afrika Kusini ikiwa tayari kuwa na uhusiano wa kibiashara na Marekani, ushuru uliowekwa unatia wasiwasi na utakua ni kikwazo kwa biashara na maendeleo ya pamoja,” imesema ofisi ya Rais.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us