UTURUKI
2 dk kusoma
Uwanja wa Ndege wa Istanbul unakuwa wa kwanza Ulaya kuzindua ndege tatu kuruka kwa wakati mmoja
“Hii siyo tu mara ya kwanza kwa Uturuki, bali katika sekta ya anga barani Ulaya. Baada ya Marekani, Uturuki ndio nchi pekee ambayo imeanzisha utaratibu huo,” amesema Waziri.
Uwanja wa Ndege wa Istanbul unakuwa wa kwanza Ulaya kuzindua ndege tatu kuruka kwa wakati mmoja
Uwanja wa ndege wa Istanbul /AA
17 Aprili 2025

Uwanja wa Ndege wa Istanbul nchini Uturuki, ambao ni wa pili kwa ukubwa katika bara la Ulaya mwaka jana, umeanzisha utaratibu wa ndege tatu kuruka kwa wakati mmoja.

Kutokana na miundombinu hiyo, Uwanja wa Istanbul unakuwa wa kwanza katika bara la Ulaya kuwa na njia tatu na ya pili duniani baada ya Marekani.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul, Waziri wa Uchukuzi wa Uturuki Abdulkadir Uraloglu, amesema Alhamisi kwamba, ndege tatu zitaweza kutua na kuruka kwa wakati mmoja katika njia tofauti.

“Hii sio tu ni mara ya kwanza kwa Uturuki, bali pia ni katika sekta ya anga barani Ulaya, lakini ni tukio la kusherehekea katika sekta ya anga ya dunia. Baada ya Marekani, Uturuki ndio nchi pekee ambayo imeanzisha utaratibu huu,” amesema.

Uraloglu amesema kwamba Uwanja wa Ndege wa Istanbul, mradi wenye maono wa Uturuki, umekuwa kivutio cha dunia tangu kufunguliwa Oktoba 29, 2018.

“Ukiwa na uwezo wa kupokea wasafiri milioni 90 kwa mwaka, Uwanja wa Ndege wa Istanbul umeisukuma Uturuki katika sekta ya anga ya dunia. Ujenzi huu wa kisasa, ambao unapokea mamilioni ya abiria, umetangaza uwezo wa kiuchumi na kitamaduni wa Uturuki kwa dunia na kuisaidia kuwa mdau muhimu katika sekta ya anga.

Uwanja wa ndege mkubwa Ulaya na wa pili kwa kupokea wageni

“Uwanja wa ndege umepokea zaidi ya wasafiri milioni 52 mwaka 2019, mwaka wake wa kwanza kutumika, na kuhudumia zaidi ya wasafiri milioni 76 mwaka 2023.

Katika orodha ya viwanja vya ndege vikubwa, ambavyo vinahudumia zaidi ya wasafiri milioni 40 kila mwaka, uwanja wa ndege umepokea wasafiri milioni 80.1, na kuifanya kuwa wa pili Ulaya na wa saba duniani.”

Uraloglu ameongeza kusema kuwa, na mfumo huu, nafasi ya Uwanja wa Ndege wa Istanbul Ulaya itaongezeka zaidi, na Uturuki kwa mara nyingine itaonesha uwezo wake wa kuongoza katika sekta ya anga na duniani kwa jumla.

Uwanja wa Ndege wa Istanbul, kwa mwaka 2024 umehudumia zaidi ya wasafiri milioni 80, na kuufanya uwanja mkubwa wa ndege Ulaya na wa pili kwa kutumika sana, kwa mujibu wa takwimu kutoka Kurugenzi Kuu ya Taifa ya Viwanja vya Ndege (DHMI).

Pia imekuwa ni kitovu cha mizigo barani Ulaya mwaka jana, kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya Baraza la Viwanja vya Ndege vya Kimataifa.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us