UTURUKI
2 dk kusoma
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki akutana na mawaziri wa Urusi na Kazakh kando ya mkutano wa BRICS
Hakan Fidan, Sergey Lavrov wamejadili masuala ya mataifa mawili, siasa na uchumi, pamoja na ushirikiano katika sekta ya nishati wanajadili masuala ya kikanda kama vile kuongezeka kwa uchokozi wa Israel, na yanayojiri huko Gaza.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki akutana na mawaziri wa Urusi na Kazakh kando ya mkutano wa BRICS
Fidan an Lavrov wamejadili masuala ya mataifa mawili, siasa na uchumi, pamoja na ushirikiano katika sekta ya nishati / AA
8 Julai 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov pembezoni mwa mkutano wa kilele wa BRICS unaoendelea mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Fidan na Lavrov walijadili masuala ya mataifa mawili, siasa na kiuchumi, pamoja na ushirikiano katika sekta ya nishati, siku ya Jumatatu, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia.

Mawaziri hao pia walibadilishana maoni kuhusu masuala ya kikanda, ikiwa ni pamoja na hatari zinazoletwa na kuongezeka kwa uchokozi wa Israel katika eneo hilo, matukio ya hivi karibuni huko Gaza, shughuli za nyuklia za Iran, na hali ya Afghanistan, vyanzo viliongeza.

Fidan pia alikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Kazakhstan na Waziri wa Mambo ya Nje Murat Nurtleu siku ya Jumatatu nchini Brazil, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.

Mkutano wa kilele wa siku mbili wa BRICS ulianza Jumapili, ukiwaleta pamoja viongozi kutoka mataifa makubwa yanayoinukia kiuchumi ili kujadili usalama wa kimataifa, mageuzi ya utawala bora, na ushirikiano katika na nchi zinazoendelea maarufu (Global South).

Kundli la BRICS linajumuisha Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini kama wanachama wa muda mrefu, pamoja na nchi kadhaa zilizojiunga hivi majuzi kwenye kundi hilo.

Uturuki imetuma maombi ya kujiunga na BRICS, na ilipata mwaliko maalumu kwa mkutano wa kilele wa mwaka huu.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us