10 Julai 2025
Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza nia yake ya kukutana na Marais Paul Kagame wa Rwanda na Felix Tshisekedi wa DRC ndani ya wiki chache zijazo ndani ya Ikulu ya White House nchini Marekani.
Uamuzi huo unafuatia hatua ya nchi hizo mbili, kusaini mkataba wa amani Juni 27, 2025, jijini Washington.
Hatua hiyo inakuja wakati Waziri Mkuu wa Israel, akimpigia chapuo Donald Trump, kushinda tuzo ya amani ya Nobel.
“Ndani ya wiki chache zijazo, viongozi wa nchi hizo mbili watakuja kusaini mkataba wa mwisho,” alisema Trump, wakati akiwa mwenyeji wa baadhi ya marais wa Afrika ndani ya Ikulu ya White House.
Aliuita mkataba huo kama hatua kubwa ambayo iliyofikiwa.