Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasili nchini Uholanzi siku ya Jumane, tayari kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa NATO jijini The Hague.
Erdogan aliwasili katika uwanja wa ndege wa Schiphol mjini Amsterdam na kukaribishwa na maofisa wa nchi hiyo, akiwemo balozi wa Uturuki ndani ya NATO Basat Ozturk, na balozi wa Uturuki huko The Hague, Selcuk Unal.
Kiongozi huyo alisafiri hadi The Hague, eneo ambalo limeandaliwa kwa mkutano huo.
Walioambatana na Rais Erdogan ni pamoja na mke wa rais Emine Erdogan, Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan, Waziri wa Ulinzi Yasar Guler, Mkuu wa Kitengo cha Intelijensia (MIT) Ibrahim Kalin, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Uturuki Fahrettin Altun, na Akif Cagatay Kilic, ambaye ni mshauri mkuu wa masuala ya mambo ya nje na usalama wa Rais Erdogan.
Wakati wa mkutano huo, Erdogan anatarajiwa kufanya mikutano kadhaa na viongozi mbalimbali ambayo itaangazia vitisho dhidi ya umoja huo.
Mkutano huo wa siku mbili, utahitimishwa siku ya Jumatano.