Rais wa Marekani Donald Trump ameitishia Iran dhidi ya kulipiza kisasi, akisema Marekani "itafuata" malengo mengine nchini Iran baada ya mashambulio ambayo alisema "ilifuta" maeneo ya nyuklia ya Iran.
"Kutakuwa na amani au kutakuwa na janga kwa Iran zaidi kuliko tulivyoshuhudia katika siku nane zilizopita," Trump alisema katika hotuba yake ya kitaifa katika Ikulu ya White House mapema Jumapili.
"Muda mfupi uliopita, jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi makubwa ya usahihi kwenye vituo vitatu muhimu vya nyuklia katika utawala wa Iran, Fordow, Natanz, na Esfahan. Kila mtu alisikia majina hayo kwa miaka mingi walipokuwa wakijenga biashara hii ya uharibifu wa kutisha," Trump alisema.
"Lengo letu lilikuwa kuharibu uwezo wa Iran wa kurutubisha nyuklia na kukomesha tishio la nyuklia linaloletwa na taifa nambari moja duniani linalofadhili ugaidi," aliongeza.
Trump alitaja mashambulizi ya Marekani "mafanikio ya ajabu ya kijeshi." Ameongeza kuwa: Nyenzo muhimu za kurutubisha nyuklia za Iran zimefutiliwa mbali kabisa.
Rais wa Marekani aliita Iran "mnyanyasaji wa Mashariki ya Kati", akisema Tehran "lazima sasa ifanye amani".
"Ikiwa hawatafanya hivyo, mashambulizi ya baadaye yatakuwa makubwa zaidi na rahisi zaidi."
Iran imelaani shambulio hilo na kuonya kuhusu ‘’matokeo makubwa’’.