Kundi la kigaidi la al-Shabaab limedhibiti Adan Yabaal, mji ulioko katika eneo la Shabelle, siku ya Jumatano kufuatia mapigano makali na jeshi la Somalia.
"Kundi hilo limeshambulia kambi za wanajeshi wa Somalia usiku wa kuamkia leo na katika maeneo ya mjini pia, kulazimisha jeshi kurudi nyuma baada ya mapigano makali," afisa mmoja wa usalama aliliambia shirika la habari la Anadolu kwa njia ya simu, akizungumza kwa masharti ya kutotambulishwa kutokana na kuwa hawaruhusiwi kuzungumza na vyombo vya habari.
Inawezekana pande zote mbili watu wamepoteza maisha, lakini idadi kamili ya waliouawa haijulikani.
Adan Ayabaal ni mji ulioko katika eneo la Shabelle, kilomita 245 kutoka mji mkuu, Mogadishu.
Mji wa kimkakati
Mji huo una umuhimu wa kimkakati kijeshi na unaunganisha jimbo la Hirshabelle na lile la jirani la kati la Galmudug.
Wakati wa operesheni ya kijeshi ya 2022, jeshi, likiungwa mkono na wapiganaji wa eneo hilo, lilifanikiwa kuukomboa kutoka kwa kundi la kigaidi la al-shabaab lenye ushirikiano wa na al-Qaeda.
Somalia imekuwa na ukosefu wa usalama kwa miaka kadhaa, huku tishio kubwa likitoka kwa makundi ya kigaidi al-Shabaab na Daesh.
Al-Shabaab imekuwa ikipigana na serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 16 na mara nyingi wanalenga maafisa wa serikali na wanajeshi.