24 Juni 2025
Mabingwa hao wa bara Ulaya ndiyo wameibuka wa kwanza katika kundi B na sasa watacheza na waliomaliza nafasi ya pili kwenye kundi A Inter Miami.
Goli lao la kwanza lilifungwa katika dakika ya 35 na mchezaji Khvicha Kvaratskhelia.
Waliongeza goli lao la pili baada ya pasi ndefu ya Bradley Barcola kumfikia Achraf Hakimi katika dakika ya 65.
PSG walijitahidi na mara nyingi walikuwa wanamiliki mchezo huo dhidi ya Seattle Sounders.
Fursa waliyoipata timu mwenyeji Sounders ni wakati Gianluigi Donnarumma alivyompa pasi Jesus Ferreira, lakini hawakufanikiwa kupata goli.
Timu nyingine iliyofuzu kwa raundi ya 16 kutoka kwenye kundi B ni Botafogo ya Brazil. Atletico Madrid ya Hispania na Seattle Sounders ya Marekani wameyaaga mashindano hayo.