18 Aprili 2025
Serikali ya Uganda inakusudia kupitisha sheria itakayoruhusu mahakama za kijeshi kusikiliza kesi za raia kwa kesi maalumu licha ya Mahakama ya Juu nchini humo kupinga hatua hiyo Januari 31, 2025.
"Sheria hiyo, ambayo itafafanua “hali ya kipekee ambayo raia anaweza kuhukumiwa kwa sheria ya kijeshi,” imeandaliwa na inasubiri idhini ya baraza la mawaziri kabla ya kuwasilishwa bungeni," Nobert Mao, Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba aliliambia Bunge.
Serikali inashinikiza kuifufua kupitia Mswada wa UPDF (Marekebisho) wa 2025.
Iwapo itapitishwa, sheria hiyo mpya itaruhusu serikali kumrudisha mpinzani Kizza Besigye kwenye mahakama ya kijeshi.
Kizza Besigye anashikiliwa na serikali ya Uganda kwa tuhuma za uhaini na umiliki wa silaha bila kibali.