AFRIKA
2 dk kusoma
Mali yafunga ofisi za kampuni ya madini ya Canada kufuatia mvutano kuhusu kodi
Barrick Gold inasema ilitia saini makubaliano yaliyowasilishwa na serikali ya Mali mwezi Februari, lakini serikali ikashindwa kutekeleza.
Mali yafunga ofisi za kampuni ya madini ya Canada kufuatia mvutano kuhusu kodi
Kufungwa kwa ofisi za kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kumesababisha mvutano kati ya shirika hilo na serikali. /AFP
16 Aprili 2025

Mamlaka nchini Mali zimefunga ofisi za kampuni ya uchimbaji madini ya Canada Barrick Gold katika mji mkuu, Bamako, kutokana na madai ya kutolipa kodi.

Ni hali inayojitokeza ya hivi sasa kuhusiana na mvutano juu ya mapato ya uchimbaji madini.

Katika taarifa Barrick ilithibitisha kuwa idara kadhaa za serikali wiki hii zilifunga ofisi zake za Bamako na kutishia kuchukua usimamizi wa mgodi uliosimamisha shughuli zake wa Loulo-Gounkoto hadi pale uchimbaji kwenye mgodi huo utakapoanza tena na kodi kulipwa.

Kampuni hiyo ya uchimbaji madini yenye makao yake makuu mjini Toronto na Mali wamekuwa wakivutana tangu 2023 kuhusu utekelezaji wa kanuni mpya ya madini ya nchi hiyo inayoipa serikali ya Mali hisa kubwa zaidi kwa uchimbaji madini ya dhahabu.

Makubaliano yaliyotiwa saini

Pande zote mbili zimekuwa zikishauriana kwa lengo la kumaliza mzozo huo.

Katika taarifa siku ya Jumanne, Barrick ilisema kuwa imetia saini makubaliano yaliyowasilishwa na serikali ya Mali mwezi Februari, lakini serikali imeshindwa kutekeleza makubaliano hayo.

"Matokeo yake sasa inaonekana kuna watu wachache ambao wanaangalia zaidi maslahi yao binafsi na ya kisiasa na kupinga mpango huu badala ya kuzingatia maslahi ya muda mrefu ya Mali na watu wake," kampuni hiyo ilisema.

Barrick inasema iko tayari kutekeleza sehemu yao ya makubaliano hayo na pia wako tayari kuanza tena shughuli zao za uchimbaji madini.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us