AFRIKA
2 dk kusoma
Urusi yaahidi msaada zaidi wa kijeshi kwa Burkina Faso, Niger na Mali
Nchi hizo za Sahel ambazo vimevitimua vikosi vya magharibi, zinazidi kujiegesha na Urusi kwa msaada wa ulinzi.
Urusi yaahidi msaada zaidi wa kijeshi kwa Burkina Faso, Niger na Mali
Mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov kukutana na mawaziri wa Muungano wa nchi za Sahel uliofanyika Moscow. / Reuters
4 Aprili 2025

Urusi imejadili njia ya kukuza uhusiano wa kijeshi na nchi za Sahel, na kuahidi kutoa mafunzo kwa vikosi vya jeshi na silaha katika hatua ya kutaka kupanua ushawishi wake kwa nchi za magharibi ambazo zilivitimua vikosi vya Ufaransa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov amesema Alhamisi baada ya mazungumzo na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa Mali, Burkina Faso na Niger kwamba Moscow iko tayari katika kusaidia kuimarisha majeshi ya nchi hizo na vikosi vya ulinzi.

“Nimesisitiza kuwa Moscow iko tayari kusaidia kupanua uwezo wa muungano wa vikosi vya pamoja vya Sahel, kuimarisha uwezo wa kupambana wa jeshi la nchi tatu na kuwapa mafunzo vikosi vyao na walinda sheria,” amesema Lavrov, na kuongeza kwamba Urusi pia inaweza kutoa vifaa vya jeshi.

‘Tuna mtizamo unaofanana’

Mwanadiplomasia huyo wa Urusi pia ameituhumu Ukraine kwa kuzorotesha hali ya utulivu wa kanda, akisema, bila kutoa ushahidi, kwamba, “Ukraine inaunga mkono wazi wazi makundi ya kigaidi katika eneo hilo la Afrika huku wadhamini wake kutoka nchi za Magharibi wakifumbia macho.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop ametilia mkazo kauli ya Lavrov, kwa kusema kuwa nchi yake inaiona Ukraine kama “taifa la kigaidi.”

“Tuna maoni yanayofanana katika kupambana na ugaidi katika eneo letu, ambao unaungwa mkono na nchi za kigeni,” amesema.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us