AFRIKA
3 dk kusoma
Maelfu ya watu waondolewa Darfur huku wapiganaji wakichukua udhibiti wa kambi ya Zamzam
Mapigano karibu na kambi na maeneo mengine yamesababisha vifo vya raia zaidi ya 300, ikiwemo wafanyakazi 10 wa shirika la misaada la Relief International.
Maelfu ya watu waondolewa Darfur huku wapiganaji wakichukua udhibiti wa kambi ya Zamzam
Wapiganaji wa RSF wamechukua udhibiti wa kambi ya Zamzam baada ya mapigano ya siku nne. Serikali na mashirika ya misaada inasema mamia ya watu wameuawa na wengine kujeruhiwa. /Reuters
16 Aprili 2025

Watu kutoka nyumba kati ya 60,000 na 80,000 - au hadi 400,000 - wamelazimika kuondoka katika kambi ya Zamzam Darfur Kaskazini nchini Sudan baada vikosi vya RSF kuchukua udhibiti wa kambi hiyo, hii ni kulingana na takwimu za shirika linalohusika na uhamiaji la Umoja wa Mataifa.

Vikosi vya RSF vilichukua udhibiti wa kambi hiyo baada ya mapigano ya siku nne ambayo serikali na mashirika ya misaada inasema yalisababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kujeruhiwa.

Siku ya Jumatatu Umoja wa Mataifa ulisema kuwa takwimu za awali kutoka kwa vyanzo vya maeneo hayo zinaonesha kuwa zaidi ya raia 300 waliuawa katika mapigano karibu na kambi za Zamzam na Abu Shouk siku ya Ijumaa na Jumamosi pamoja na mji wa Al Fasher Darfur Kaskazini.

Idadi hii inajumuisha wafanyakazi 10 wa shirika la misaada la Relief International, ambao waliuawa katika moja ya kituo pekee cha afya kilichokuwa kimebaki ndani ya kambi ya Zamzam, alisema msemaji wa Umoja wa Mataifa.

Kwa muda mrefu mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya kuhusu ukatili iwapo RSF wangefanikiwa kuchukua udhibiti wa kambi hiyo ambayo watu walikuwa wanakabiliwa na njaa kali, na iliokuwa karibu na ngome pekee ya jeshi la Sudan, Al Fasher katika eneo la Darfur.

Picha za setlaiti kutoka Maxar Technologies zinaonesha nyumba zikiungua na moshi ukifuka katika kambi ya Zamzam siku ya Ijumaa, ishara ya kama mashambulio ya awali ya RSF.

RSF imekanusha madai hayo na wanasema kambi ya Zamzam ilikuwa inatumika kama ngome ya makundi yanayounga mkono jeshi la serikali.

Mapigano ya ndani

Wakati vita vikianza, kambi hii ilikuwa na watu karibu laki tano, idadi hiyo inaaminika kuongezeka maradufu.

Katika video iliyosambazwa na wapiganaji wa RSF, naibu mkuu wa vikosi hivyo Abdelrahim Dagalo anaonekana akizungumza na kundi dogo la watu waliokimbia makazi yao, na kuwaahidi chakula, maji, huduma za matibabu na kurejeshwa katika maeneo yao.

RSF iliendeleza mashambulizi yake kwenye kambi hiyo baada ya jeshi kuchukua udhibiti wa mji mkuu, Khartoum, kujihakikishia mafanikio yake ya kuwepo kote katikati mwa nchi.

Pia RSF imezidisha mashambulio ya kutumia ndege zisizo na rubani katika maeneo ya jeshi, ikiwemo kushambulia kituo cha kufua umeme cha Atbara kaskazini mwa nchi siku ya Jumatatu, kulingana na shirika la taifa la umeme, na kusababisha kukatika kwa umeme katika sehemu ambayo ambayo ilikuwa makao makuu ya nchi kwa muda Port Sudan.

Vita nchini Sudan vilianza Aprili 2023, chanzo kikiwa mvutano wa utawala kati ya jeshi na RSF, jambo lililokatisha tamaa matumaini ya kupata serikali ya kiraia.

Mapigano hayo yamelazimisha mamilioni ya watu kukimbia makazi yao na kuharibu maeneo mengi ya nchi, pamoja na kuwepo kwa ukame katika sehemu mbalimbali.

CHANZO:REUTERS
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us