Tangazo hilo la chama cha NRM, ni thibitisho la kwanza rasmi kuwa Museveni yuko kwenye kinyang’anyiro hicho. Mpinzani wa muda mrefu wa Museveni, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, pia naye anajiandaa kugombea tena baada ya kulalamika kuhusu matokeo ya uchaguzi wa 2021.
Uchaguizi wa Uganda unaotarajiwa kufanyika mwezi Januari utakuwa uchaguzi mkuu ambapo wapiga kura watachagua rais na wabunge.
Museveni, ambaye amekuwa uongozini tangu 1986, ni mmoja katika ya viongozi waliokuwepo madarakani kwa muda mrefu barani Afrika. Chama tawala kimebadilisha katiba mara mbili kumruhusu aendelee kugombea urais.
Mpinzani wake mkuu, Robert Kyagulanyi, pia anajianadaa kugombea, baada ya kuwania urais 2021. Kyagulanyi alikataa matokeo ya uchaguzi uliopita, akidai kuchakachuliwa kwa matokeo na maafisa wa usalama kuingilia kati. Hata hivyo, Museveni, anasema kuwepo kwake kwa muda mrefu uongozini ni kutokana na kuungwa mkono na watu wengi.