Kwa muda wa wiki moja, Mohamed mwenye umri wa miaka minane amekuwa akiugua maumivu ya mkono kufuatia shambulio la makombora. Lakini ni mmoja wa waliobahatika katika mji wa magharibi mwa Sudan wa El-Fasher, ambao unakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo.
"Mmoja wa majirani zetu alikuwa muuguzi. Alitusaidia kuzuia damu isivuje," babake Mohamed, Issa Said, 27, aliliambia shirika la habari la AFP kupitia uunganisho wa satelaiti chini ya kukatika kwa jumla kwa mawasiliano.
"Lakini mkono wake umevimba na hawezi kulala usiku kutokana na maumivu."
Kama inakadiriwa kuwa watu milioni moja zaidi waliokwama jijini wakiwa wamezingirwa mwaka mzima na wapiganaji wa kikosi cha RSF, Said hawezi kufika hospitalini kwa ajili ya huduma ya dharura.
Hospitali ya Saudia pekee ndio imebakia
Huku kukiwa na vifaa duni tu vilivyobaki katika mji wa El-Fasher, familia yake ni miongoni mwa wale ambao msaada wao pekee wa kimatibabu umetoka kwa majirani na wanafamilia ambao wanafanya maarifa.
Katika harakati zake za kuuteka mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini -- mji mkuu pekee wa Darfur ambao haujawahi kudhibitiwa kwa kipindi cha miaka miwili ya vita na jeshi la Sudan -- RSF imeanzisha mashambulizi juu ya mashambulizi, ambayo yamekabiliwa na jeshi na vikosi vinavyounga mkono wanajeshi.
Hata kama watu wangethubutu barabarani, Hospitali ya Saudia ndiyo pekee inayofanya kazi kwa kiasi sasa, kulingana na chanzo cha matibabu huko, na hata hiyo imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara.
Shughuli za kutoa misaada huko El-Fasher zimetatizika pakubwa kutokana na "vikwazo vya ufikiaji, uhaba mkubwa wa mafuta na mazingira tete ya usalama," huku huduma za afya zikiathirika haswa, shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia misaada OCHA lilisema.
Kutumia mitishamba kutibu waliojeruhiwa
Mohamed, mratibu wa misaada ambaye alikimbilia El-Fasher baada ya kupigwa risasi kwenye paja wakati wa shambulio la RSF siku zilizopita kwenye kambi ya karibu iliyokumbwa na njaa ya Zamzam, anakadiria mamia ya raia waliojeruhiwa wamekwama katika jiji hilo.
Kulingana na vyanzo vya misaada, maelfu wamekimbia Zamzam kuelekea mji huo, ambao tayari unakumbwa na njaa kubwa kulingana na tathmini iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo watu wa El-Fasher "wamefungua nyumba zao kwa waliojeruhiwa," Mohamed ameiambia AFP, akiomba kutambuliwa tu kwa jina lake la kwanza kwa sababu za kiusalama.
“Ukiwa na fedha unamtuma mtu akanunue shashi safi au dawa za kutuliza maumivu akipata, lakini lazima ufanye na ulichonacho,” alisema Mohamed ambaye jeraha lake la mguu lilimaanisha kubebwa umbali wa kilomita 15 (maili tisa) kutoka Zamzam hadi mjini, safari iliyochukua saa kadhaa.
Hali mbaya ya jehanamu
Katika vyumba vya kuishi na jikoni vilivyojaa watu, raia ambao hawana mafunzo yoyote ya matibabu hushirikiana katika kuandaa utaratibu wa huduma ya dharura, wakitumia vifaa vya nyumbani na mitishamba kutibu majeraha ya moto, majeraha ya risasi na majeraha ya mabomu.
Mwathiriwa mwingine, Mohamed Abakar, 29, alisema alikuwa akichota maji kwa ajili ya familia yake wakati risasi ilipopenya hadi mguuni kwake.
Mara moja kiungo hicho kilivunjika chini yake, na jirani yake akamkokota hadi nyumbani kwake, akimtengenezea banzi kutoka kwa vipande vichache vya mbao na nguo.
"Hata kama itaponya mguu wangu uliovunjika, risasi bado iko ndani," Abakar aliiambia AFP, pia kwa kiungo cha satelaiti.
Kufikia Jumatatu, mashambulizi ya hivi majuzi ya RSF dhidi ya El-Fasher na kambi zinazozunguka kambi za wakimbizi yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 400, kulingana na Umoja wa Mataifa.