10 Julai 2025
Hiyo ina maana kwamba mimi au wewe tunaweza kuwa miongoni mwao.
Utafiti mpya unaonyesha kwamba iwapo hakutakuwa na mabadiliko makubwa katika mfumo wa maisha, basi takriban asilimia 60 ya watu duniani kufikia mwaka 2050 watakuwa na unene wa kupitiliza.
Takwimu zinatabiri kwamba theluthi moja ya vijana wanene wanaweza kutoka Afrika Kaskazini, Mashariki ya Kati, Amerika Kusini na nchi za Karibiani.
Lakini sio hilo tu, utafiti unataka hatua zaidi zichukuliwe ili kubadilisha mifumo ya afya kote ulimwenguni.