ULIMWENGU
5 DK KUSOMA
Mgogoro kati ya Palestina na Israel
Mgogoro kati ya Palestine na Israel ni wa muda mrefu kuwahi kutokea duniani, ambao umeanza mwanzoni mwa miaka ya 1900
Mgogoro kati ya Palestina na Israel
Mgogoro wa Israel na Palestine ulianza miaka ya 1900 / Picha: AFP
13 Oktoba 2023

Mgogoro kati ya Palestine na Israel ni wa muda mrefu kuwahi kutokea duniani, ambao umeanza mwanzoni mwa miaka ya 1900, ambapo kundi dogo la Mayahudi Wazungu walipotaka kuanzishwa kwa makazi ya Mayahudi.

Mwaka 1917, aliyekuwa wakati huo, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Arthur Balfour, aliandika barua kwa Lionel Walter Rothschild, kiongozi wa jamii ya Mayahudi wa Uingereza.

Katika barua hiyo, Balfour alionyesha dhamira ya serikali ya uingereza ya kusaidia “kuanzishwa kwa makazi ya mayahudi katika eneo la Palestine.”

Barua hiyo, tangu enzi, imekuwa ikijulikana kama Makubaliano ya Balfour. Mnamo mwaka 1922, Umoja ya Mataifa ya wakati huo ambayo ilikuwa ikifahamika kama ‘The League of Nations’ iliipa Uingereza mamlaka ya kutawala eneo ambalo wakati huo liliitwa Palestine.

Ambayo leo hii, ni Israel pamoja na Ukingo wa Magharibi na Gaza.

Wakati wa utawala huo, Uingereza iliruhusu wimbi la wahamiaji wa kiyahudi kuingia Palestine na kuanza kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa taifa ya kiyahudi katika ardhi ya Palestine.

Uhamiaji wa Wayahudi katika ardhi ya Palestine kati ya vurugu za mara kwa mara kati ya mayahudi na waaarabu.

Taifa la Israel laundwa rasmi

Mwezi Mei, tarehe 14, 1948, Uingereza ilimaliza utawala wake Palestine kufuatia makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya mwaka wa 1947, ambayo yalitaka kugawanywa kwa eneo hilo kati ya Waarabu na Wayahudi.

Siku hiyo hiyo, taifa la Israel liliundwa kwa eneo lililopewa Wayahudi kwa mujibu wa Mpango wa kuligawa.

Vita vya kwanza vya Waarabu-Wayahudi viliibuka baada ya kuanzishwa kwa taifa la Israel. Vilijumuisha nchi kadhaa zikiwemo Misri, Syria, Jordan, Iraq na Lebanon. Waarabu walishindwa vita.

Zaidi ya vijiji 500 vya Palestine na miji ilibomolewa. Wapalestina wanaokisiwa kufika 750,000 walilazimika kukimbia makazi yao, Wapalestina ghafla wakawa hawana utaifa, na ardhi ambayo ilikuwa inaitwa Palestine kabla ya 1948 ikawa ndio Israel ya leo.

Mgogoro waendelea

Mgogoro kati ya Palestine-Israeli ukaendelea kuwa mgumu zaidi. Israel ilipigana vita vinne zaidi dhidi ya Waarabu (mwaka 1956, 1967, 1973 na 1982) na mara zote hizo, wamekuwa wakiibuka washindi.

Waarabu, ambao walikataa mpango wa kuigawa Palestine mwaka 1948, hivi sasa wapo tayari kuukubali eneo pekee walilopoteza katika vita vya Siku Sita vya mwaka 1967, lijulikanalo Gaza, Ukingo wa Magharibi na Mashariki mwa Jerusalem.

Jitihada zote za amani kati ya Israel na Palestine kwa namna fulani ziliwekwa pembeni baada ya kutoleta tija baada ya pande zote zinazozozana kuendelea kujikita katika mzozo.

Utekelezaji wa jitihada hizo ulikuwa mgumu kwa sababu haukujadili kiini cha mgogoro ambacho ni uhuru wa Palestina, Jerusalem na kurudi kwa wakimbizi, wanaokisiwa kufikia milioni sita.

Leo hii, Wapalestina waliopo Israel ni asilimia 21 ya idadi ya watu wote milioni 9.73.

Mwaka 1987, vuguvugu maarufu ijulikanayo duniani kama Intifada ya kwanza iliibuka Gaza dhidi ya Israel kukalia maeneo ya Ukingo wa Magharibi, Gaza na Jerusalem.

Jitihada za makubalino ya amani

Vuguvugu hiyo iliisha baada ya kusainiwa kwa Makubaliano ya Oslo mwaka 1993 kwa kuundwa kwa Mamlaka ya Palestina kama serikali ya mpito huku ikiwa na mipaka ya kujitawala hasa katika maeneo ya mjini ya Ukingo wa Magharibi na Gaza.

Hata hivyo, Israel ndio inadhibiti hali ya usalama na uamuzi wa kufanya mashambulizi wakati wowote.

Mwaka 1995, Israel ilijenga uzio wa umeme na ukuta wa zege kuzunguka Gaza, ikidhibiti harakati zote katika eneo la Palestina liligawanywa.

Hamas ikapata umaarufu muda mfupi mwaka 1987 baada ya mapambano ya kwanza dhidi ya kukaliwa na Israel kwa eneo la Ukingo wa Magharibi, Gaza na Mashariki mwa Jerusalem.

Kundi hilo linapinga Makubaliano ya Amani ya Oslo, halitambui utaifa wa Israel lakini linatambua taifa la Israel kulingana na mipaka yam waka 1967.

Kundi hilo liliunda kitengo cha jeshi kinachoitwa Izz al-Din al-Qassam kufanya mapambano ya kijeshi dhidi ya Israel.

Imekuwa ikidhibiti Gaza tangu mwaka 2007, eneo ambalo lina kilomita za mraba na makazi ya zaidi watu milioni mbili, baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2006.

Juni, mwaka 2007, Israel iliweka vizuizi vya ardhini, anga, na majini dhidi ya Gaza, na mara kwa mara kufanya mashambulizi dhidi ya Hamas, na kuwazuia zaidi ya watu milioni mbili katika kile Palestine inachokiita jela ya wazi.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us