MICHEZO
1 DK KUSOMA
Marefa kutoka Rwanda kuchezesha mchezo wa fainali ya CAF kwa wanawake
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeorodhesha majina ya waamuzi wa watatu.
Marefa kutoka Rwanda kuchezesha mchezo wa fainali ya CAF kwa wanawake
Mwamuzi Salma Mukansanga wa Rwanda./Picha: Wengine / Others
24 Oktoba 2024

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeorodhesha majina ya Aline Umutoni, Alice Umutesi na Salma Mukansanga kama waamuzi watakochezesha fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo zitatimua vumbi kati ya Novemba 2 hadi 8, nchini Morocco.

Umutoni alichaguliwa kama mwamuzi wa kati wakati Umutesi atakuwa mwamuzi msaidizi, atakuwa kwenye chumba maalumu cha VAR.

Michuano ya za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa wanawake inashirikisha timu nane zikiwemo Aigles de la Medina ya Senegal, EDO Queens kutoka Nigeria na University of the Western Cape ya Afrika Kusini.

Nyingine ni Tutankhamun ya Misri, CBE FC ya Ethiopia, Mameodi Sundowns kutoka Afrika Kusini, ASFAR ya Morocco na TP Mazembe kutoka DRC.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us