AFRIKA
2 dk kusoma
Serikali ya muungano Afrika Kusini hatarini baada ya mjumbe kushindwa kwenda Marekani
Washirika wakuu wa serikali ya muungano ya Afrika Kusini ANC na DA wametofautiana kuhusu namna ya kukabiliana na ushuru wa serikali ya Trump.
Serikali ya muungano Afrika Kusini hatarini baada ya mjumbe kushindwa kwenda Marekani
Vyama vya ANC na DA viliungana baada ya ANC kushindwa kupata wingi wa wabunge katika uchaguzi wa 2024. / Reuters
17 Julai 2025

Washirika wakuu wa serikali ya muungano ya Afrika Kusini wametofautiana kuhusu namna ya kukabiliana na ushuru wa serikali ya Trump, baada ya chama hicho kidogo kusema kuwa mjumbe wa rais amenyimwa viza ya kusafiri Marekani kufanya mashauriano na nchi hiyo.

Chama cha Democratic Alliance kimesema siku ya Jumanne kuwa Marekani imemkataa rasmi mpatanishi aliyeteuliwa na Rais Cyril Ramaphosa, Mcebisi Jonas, na kumnyima viza ya kidiplomasia mwezi Mei.

Chama cha DA hakijatowa ushahidi wowote kuhusu madai hayo, ambayo afisa wake wa masuala ya uhusiano wa kimataifa Emma Louise Powell alirudia katika taarifa siku ya Alhamisi.

Katika kujibu hilo, msemaji wa rais, Vincent Magwenya, hakuweka wazi kama Jonas alinyimwa viza.

Hakuwa miongoni mwa ujumbe wa Marekani Mei 2025

"Rais Ramaphosa hajakuwa na haja ya Bwana Jonas kufanya ziara Marekani kwa shughuli muhimu," alisema katika taarifa.

Aliongeza kuwa Jonas amekuwa akifanya kazi kimya kimya na wizara za biashara na mambo ya nje. Tangu kuteuliwa kwake mwezi Aprili, serikali haijataja kama Jonas alikutana na maafisa wowote wa Marekani.

Hakuwa miongoni mwa ujumbe uliosafiri kwenda Washington mwezi Mei, ziara ambayo Rais wa Marekani Donald Trump alimshambulia Ramaphosa katika ofisi ya rais ya Oval na madai ya "mauaji ya halaiki ya wazungu" nchini Afrika Kusini.

Hofu ya ajira kupotea

Ushuru wa asilimia 30 wa Afrika Kusini unaanza kutumika Agosti 1. Gavana wa Benki Kuu ya Afrika Kusini Lesetja Kganyago ameonya siku ya Jumatano kuwa huenda ikasababisha kupotea kwa kazi 100,000.

Chama cha Ramaphosa cha African National Congress (ANC) kimeshangazwa kuwa chama cha DA kilifanya ziara kivyake nchini Marekani mapema mwaka huu kueleza kuhusu Afrika Kusini kwa wanasiasa wa Marekani.

ANC na DA waliunda muungano ambao haukutarajiwa baada ya ANC kupoteza wingi wa viti bungeni katika uchaguzi mwaka uliopita. Lakini wametofautiana kuhusu sheria za haki, sera ya elimu na bajeti.

Ramaphosa alimfuta naibu waziri wa chama cha DA kwa kutoomba idhini katika safari yake ya kwenda Marekani.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us