AFRIKA
2 dk kusoma
AU yaridhishwa na hatua ya kusitishwa mapigano Jamhuri ya Afrika ya Kati
Umoja wa Afrika umetoa wito kwa makundi yenye silaha katika nchi hiyo "kuweka silaha zao chini na kushiriki kwa nia njema katika majadiliano ya kitaifa na maridhiano".
AU yaridhishwa na hatua ya kusitishwa mapigano Jamhuri ya Afrika ya Kati
Serikali ya rais Faustin Archange Touadera imetia saini makubaliano ya amani na makundi mawili makubwa yenye silaha. / AFP
18 Julai 2025

Siku ya Ijumaa Umoja wa Afrika umeeleza kuridhishwa kwake kwa kuvunjwa kwa makundi mawili yenye silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kutoa wito kwa makundi mengi kusalimisha silaha pia.

Nchi hiyo imekabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe tangu kupata uhuru 1960.

Licha ya makubaliano ya amani 2019 kati ya serikali na makundi ya waasi 14, bado kuna makundi mengine yanayoendelea kupigana na kudai udhibiti wa baadhi ya maeneo katika nchi hiyo.

Mwezi Aprili, serikali ilisaini makubaliano ya amani na makundi mawili makubwa: UPC na 3R.

‘Majadiliano ya kitaifa’

Katika taarifa iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf ameeleza kuridhishwa na kuvunjwa kwa makundi ya UPC na 3R, ambako kulitangazwa Julai 10 na viongozi wake.

Taarifa hiyo imetoa wito kwa makundi yote yenye silaha "kusalimisha silaha zao na kwa nia njema kujumuika katika majadiliano ya kitaifa na maridhiano".

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya hivi karibuni katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yalianza zaidi ya muongo mmoja uliopita. Serikali imeweka usalama katika miji mikubwa na machafuko yamepungua katika miaka ya hivi karibuni.

Lakini mapigano yanazuka mara kwa mara katika maeneo yaliyo mbali na miji kati ya waasi na jeshi la taifa.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us