AFRIKA
1 dk kusoma
Dola milioni 60 kwa mradi wa mafuta na gesi Mtwara, Tanzania
Tanzania inatarajia kutumia dola milioni 60 kufanikisha uchimbaji mafuta na gesi katika kitalu cha Mnazibay mkoani Mtwara kusini mwa nchi. Gharama hiyo itahusisha uchimbaji wa visima vitatu pekee ikiwa ni hatua ya kuthibitisha kiwango cha gesi
Dola milioni 60 kwa mradi wa mafuta na gesi Mtwara, Tanzania
18 Julai 2025

Hatua hii inafuatia ukamilishaji wa awali wa utiaji saini wa ushirikiano kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kampuni ya First Exploration and Petroleum Development Company (First E & P) ya Nigeria yenye lengo la kuweka rasmi muongozo wa ushirikiano wa utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa nishati hiyo.

Kulingana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (TPDC) Mussa Makame, kitalu ambacho kitafanyiwa utafiti ni kile ambacho serikali imeikabidhi TPDC ili kukiendeleza.

Hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano hayo imefanyika jijini Dodoma.

Shirikia hilo linasema kuwa pamoja na kazi zingine zilizofanyika katika kitalu hicho, jukumu kubwa sasa ni uchorongaji na uchimbaji wa kuanza kutafuta mafuta na gesi katika eneo hilo linalotajwa kuwepo kwenye bahari yenye kina kirefu.

“Kwa sasa tumeweza kuchimba eneo lenye kina cha mita 800, lakini katika uchimbaji ni jambo la kawaida kabisa kushirikiana na makampuni mengine ili kupunguza gharama na kuwezesha upatikanaji wa haraka wa gesi”, amesema Makame

Serikali ya nchi hiyo ina matumaini kuwa kupatikana kwa gesi hiyo kutasaidia uzalishaji wa umeme kwenye magari, viwanda pamoja na usambazaji wa nishati hiyo majumbani.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us