ULIMWENGU
5 dk kusoma
Mpango wa Trump wa ‘wahamiaji kuondoka kwa hiari' ni mfano wa Nakba
Nyuma ya lugha ya kidiplomasia “wahamiaji kuondoka kwa hiari” kuna sera mahsusi ya watu kutimuliwa kwa lazima na kufuta utamaduni, ikiwa mfano wa awamu mbaya zaidi ya historia ya Palestina.
Mpango wa Trump wa ‘wahamiaji kuondoka kwa hiari' ni mfano wa Nakba
Donald Trump na Benjamin Netanyahu walizindua sera mapema mwezi huu za kuita kuondoa watu kwa lazima kama ‘’kuondoka kwa hiari’’. / AP
16 Julai 2025

Gaza City, Gaza — Wiki hii jijini Washington, katika meza ya Ikulu ya Marekani ya White House, Donald Trump na Benjamin Netanyahu walikaa na kutabasamu wakiamini kama watu ambao wanahodhi hatma ya watu, ramani, na ndege za kivita.

Kama kawaida, Trump, hakuonekana kama kiongozi wa nchi lakini kama mfanyabiashara. Wakati huu, Gaza ndiyo ardhi ambayo inauzwa - au, kwa watu kutimuliwa. Trump aliwaambia waandishi wa habari: "Tumekuwa na ushirikiano mzuri kutoka kwa mataifa ya karibu... kwa hiyo kuna jambo zuri ambalo litafanyika."

"kitu kizuri."

Ndiyo hivyo wazo la Trump la kuondoa jamii nzima ya watu katika ardhi yao – na kufuta utambulisho wa watu, kufukia makaburi, na kuondoa athari za utamaduni wa miaka mingi, na kuwapeleka sehemu ambazo "ni nzuri".

Anaita uhuru, lakini iwapo utakubali kuondoka nyumbani kwako. Wapalestina waondoke katika ardhi yao waende wakaishi sehemu isiyojulikana, bila heshima au watu wa kuamiliana nao.

Inabidi uache kila kitu chako na kusema "asante" kwa wale walioharibu nyumba yako.

Ni wazi kuwa lengo ni kuendeleza vita vya Gaza — eneo lenye kilomita mraba 327 — na kutupwa vilipuzi, sababu ilikuwa kuchora ramani ya kuwaondoa watu. Iwe ni kwa lazima au kwa hiari, hilo halijalishi.

Sasa dira yao iko wazi: pale Trump na Netanyahu wanapokaa pamoja, wanazungumzia kuhusu kuwatimua watu wa Gaza. Na nani anaweza kusimamisha uwendawazimu huu?

Chini ya uongozi wa Trump, Marekani inaunga mkono wazi kufukuzwa kwa Wapalestina – kuwaondoa katika ardhi yao.

Marekani inahusika kwenye vita vya Gaza, ni kama ndiyo jambo linalowashughulisha pekee. Trump aliweka ujumbe kwenye mtandao wa twitter na kuzungumzia kuhusu suala hilo kila wakati - kila wakati akiwa upande wa Israel, kila mara akiwashtumu Wapalestina - ni kama Gaza ndiyo suala pekee aliloangazia, ardhi nzuri sana ambayo angezindua mradi wake wa kiuchumi, ambayo wakati mmoja aliiita "the Riviera”.

Trump anaona fursa.

Kinachomuunganisha yeye na watu hawa ni nini mbali na makubaliano ya silaha na Israel?

Vipi anaweza kuitwa mtu wa amani au mwenye utu wakati anawafadhili wauaji na kumpongeza wakati watoto, wanawake, na wazee wanaangamizwa?

Trump haoni Wapalestina. Anaona fursa ya kuwa shujaa wa mradi mkubwa - unaolipiwa na wageni.

Wakati akiwa Washington, Netanyahu alisema: “Kama wanataka kukaa, wanaweza kubaki. Kama wanataka kuondoka, wanaweza kwenda. Gaza haitakiwi kuwa gereza."

Lakini Israel imekataa kumaliza vita. Inaendelea kushambulia.

Kuna gereza gani baya zaidi ya mji ambao hauna maji, hauna dawa, hakuna umeme, bila amani?

Alafu unawaambia watu: "Chagua”.

Hivi ndivyo watu wanavyotimuliwa - siyo kwa kutumia nguvu, lakini kwa kuwa na chaguo moja tu la kifo.

Wanasema "wahamiaji wanaondoka kwa hiari" badala ya kulazimisha watu kuondoka; "fursa nzuri " badala ya kuangamiza; "nchi wenyeji" badala ya watu kuondolewa.

Hii si lugha ya kidiplomasia - ni lugha ya kudanganya inayotumia kuficha uhalifu mbaya , kuondoa harufu ya uvundo wake.

Kuishi maisha magumu kwa heshima


Huko Gaza, maisha si ya ushairi - ni kujaribu kuishi katika mazingira magumu kila siku.

Kila siku Wapalestina wanaskia sauti za ndege za kivita, kutafuta mkate, au kutembea bila mafuta, njia za kutafuta maji, kutafuta dawa - na bado anamfundisha mwanawe kuwa "nyumbani’’ si sehemu ya kuuzwa, hata kama kunaungua.

Wakati wa vita, watu wa Gaza wamepitia mambo magumu sana ya mateso – njaa, mauaji, watu kuondolewa, kuhamishwa, na kupoteza maisha.

Mpalestina mmoja, kati ya watano huko Gaza wanakabiliwa na njaa kulingana na shirika la IPC, huku usambazaji wa chakula ukitatizwa na mashambulio. Pamoja na hayo kila Mpalestina anang’ang’ania sehemu yake Gaza na kuwafunza watoto wake kufanya hivyo.

Kwa hiyo wakati Trump anasema nchi jirani ziko tayari, ni kama anapendekeza mama amuachie jirani mtoto wake na kuanza maisha mapya.

Janga la Nakba, linalokuja kivingine

Hili si jambo jipya - ni kama wameimarisha mpango wao wa zamani.

1948, Wapalestina zaidi ya 700,000 waliondolewa kutoka kwenye vijiji vyao, na kuwa wakimbizi na kunyimwa haki zao za kurudi licha ya azimio la Umoja wa Mataifa la 194, ambalo linataka wakimbizi wanaotaka kurudi makwao na kuishi kwa amani na majirani zake waruhusiwe kufanya hivyo.

Waliondolewa kwa mbinu na vurugu na wengine wakauawa, kukamatwa, kuteswa, na nyumba kuvunjwa - kama inavyofanyika Gaza kwa sasa.

Leo, wanatakiwa "kuchagua" kuondoka "kwa hiari yao" na kuishi katika "maeneo yenye amani". Hii ni kulingana na nyaraka za Marekani ziloonekana na shirika la Reuters Julai 7, ambazo zinaonesha mpango wa dola bilioni 2 kujenga sehemu kubwa ndani na pengine nje ya Gaza na kuandaa kuwaondoa Wapalestina.

Dunia imekaa Kimya: Inahusika katika uhalifu


Swali kuu ni: Vipi kuhusu dunia? Kwa nini imekaa kimya kuhusu mustakabali wetu wa pamoja?

Ziko wapi hotuba za kutetea haki za binadamu wakati Gaza ikishambuliwa, watu wake wakiuawa, na pia kuambiwa waondoke wakihofia kifo na njaa?

Katika suala la Ukraine, sauti zilipazwa, taasisi zikachangamka, na mateso yakageuzwa kuwa suala la kisheria, na kisiasa.

Lakini kwa Gaza, watu wako kimya.

Wakati Trump akisimama na kusema "wahamiaji kuondoka kwa hiari," hatoi suluhisho, anabadilisha kauli ya kuondoa watu na kauli ya kufanya utu.

Huku ni kucheza na lugha tu.

Kwa simulizi hii, Palestina inaandaliwa kugawanywa.

Watu kuruhusiwa kuchagua ni pale mapigano yanapositishwa, siyo watu kutakiwa kuondoka huku wanashambuliwa kwa mabomu.

Trump hazungumzii Wapalestina kama watu, lakini kama wanaopinga mradi wake. Haoni maisha kwao - anaona idadi kubwa ya watu wanaotakiwa kuongozwa kwa kuangalia maslahi yao.

Hapa, mijadala ya kikoloni inajirudia tena: ukubaliane na masharti yetu au uondoke, kwa faida yako.

Lakini kwa Mpalestina — anayezika watu wake, kuwafundisha watoto wake, kuhifadhi kumbukumbu zake — yuko kwenye makabiliano. Siyo kwamba makabiliano ni ushujaa, lakini ndiyo njia pekee ya kujilinda asije akapotea kutokana na mtazamo wa mtu mwingine.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us