MICHEZO
1 dk kusoma
Man City yaingia hatua ya mtoano kombe la dunia la klabu baada ya kuwafunga Al-Ain 6-0
Timu ya Manchester City ya Ligi Kuu ya England imefuzu katika hatua ya mtoano ya kombe la dunia la klabu baada ya kuifunga klabu ya Al-Ain ya Imarati 6-0 siku ya Jumapili.
Man City yaingia hatua ya mtoano kombe la dunia la klabu baada ya kuwafunga Al-Ain 6-0
Timu ya Manchester City. / Reuters
23 Juni 2025

Timu nyingine iliyofuzu katika hatua hiyo kutoka kundi G ni Juventus. Juventus iliwafunga Wydad Casablanca ya Morocco magoli 4-1 Jumapili.

City na Juventus watakutana kwenye mechi yao ya makundi jijini Orlando siku ya Alhamisi kubaini nani ataibuka mshindi wa kundi hilo.

Atakayemaliza wa kwanza kundi G atacheza dhidi ya atakayemaliza wa pili kwenye kundi H. Atakayekuwa wa kwanza kwenye kundi H atakabiliana na aliyemaliza nafasi ya pili kwenye kundi G.

Tayari Real Madrid ya Hispania imefuzu kwa hatua hiyo ya mtoano, sawa na Red Bull Salzburg ya Austria kutoka kwenye kundi H. Timu zingine kwenye kundi hilo ni Al-Hilal ya Saudia Arabia na Pachuca kutoka Mexico.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us