SIASA
1 dk kusoma
Uturuki ina nafasi kwa ‘amani, diplomasia na usalama wa NATO’: Altun
Akizungumza kwa njia ya video katika jopo maalumu huko Amsterdam, Fahrettin Altun amesema kuwa umoja huo unakumbana na changamoto mbalimbali kama taarifa potofu na uingiliwaji wa mataifa ya nje, akisisitiza mikakati mipya ya kimawasiliano.
Uturuki ina nafasi kwa ‘amani, diplomasia na usalama wa NATO’: Altun
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun amesisitizia nafasi ya Uturuki katika jitihada za upatikanaji wa amani duniani./Picha; Wengine / AA
23 Juni 2025

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun amesisitizia nafasi ya Uturuki katika jitihada za upatikanaji wa amani duniani, katika jopo maalumu lililofanyika mjini Amsterdam.

Katika ujumbe wake wa picha mjongeo wenye kichwa cha habari “Uturuki na NATO katika zama Maboresho ya Kiusalama na Changamoto za Taarifa”, Altun aliangazia mchango wa Uturuki katika operesheni mbalimbali za NATO, akiielezea Uturuki kama “suluhisho la amani na haki”, kikanda na ulimwenguni.

“Kama moja ya nchi ambazo zimeshiriki katika operesheni za NATO, Uturuki ina nafasi muhimu katika amani na haki na imefanya jitihada mbalimbali kufikia suala hilo,” alisema.

Tukio hilo liliandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais wa Uturuki na kufanyika katika mji mkuu wa Uholanzi.

Tukio hilo, liliwaleta pamoja watunga sera na wataalamu wengine kujadiliana masuala ya taarifa.

Altun aliangazia nafasi ya kihistoria ya NATO kama mshirika wa kiusalama tangu kuanzishwa kwake.

“Muungano huu umetuhakikishia utulivu na usalama sio ulaya tu na pande zingine za ulimwengu,” alieleza.

 Pia, aligusia mabadiliko mbalimbali yanayoendelea ulimwenguni.

“Mfumo wa kiulimwengu unapitia mabadiliko makubwa,” alisema Altun.

Akitoa mifano ya vihatarishi vya kiusalama ulimwenguni, Altun alionya kuwa uingiliwaji wa mkakati wa mawasilino ya NATO unahatarisha usalama.

 

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us