AFRIKA
3 dk kusoma
Waziri wa zamani wa Côte d'Ivoire Billon kuongoza upinzani katika uchaguzi wa Oktoba
Waziri wa zamani wa Biashara wa Côte d'Ivoire Jean-Louis Billon anasema anataka kuwakilisha chama kikuu cha upinzani katika uchaguzi wa urais wa Oktoba baada ya Tidjane Thiam kuondolewa kwenye orodha ya mwisho ya wagombea.
Waziri wa zamani wa Côte d'Ivoire Billon kuongoza upinzani katika uchaguzi wa Oktoba
Waziri wa zamani wa Biashara wa Côte d'Ivoire Jean-Louis Billon anasema ni wakati wa nchi kupata uongozi mpya sasa. / Reuters
9 Juni 2025

Waziri wa zamani wa Biashara wa Côte d'Ivoire Jean-Louis Billon anasema ana nia ya kuongoza chama cha upinzani cha PDCI katika uchaguzi wa urais wa Oktoba baada ya mkuu wa zamani wa benki ya Credit Suisse Tidjane Thiam kuondolewa kwenye orodha ya mwisho ya wagombea wiki iliopita.

Suala la nani atakayeongoza chama kikuu cha upinzani huenda likaongeza taharuki kwa nchi ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa kakao duniani, na iliyo na historia ya machafuko wakati wa uchaguzi ikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mfupi baada ya uchaguzi wa urais wa 2010 vilivyosababisha mauaji ya watu zaidi 3,000.

Katika mahojiano na shirika la habari la Reuters kwenye mji mkuu wa kibiashara Abidjan, Billon, mwenye umri wa miaka 60, alilaumu maafisa wa chama kwa namna walivyoshughulikia ugombea wa Thiam kisheria na pia kusema kuwa huenda hata akawakilisha chama kingine, ingawa alisema ilikuwa mapema kufanya maamuzi hayo.

"Naomba ridhaa ya chama cha PDCI," alisema.

'Kukosa kujiandaa'

"Rais wa (PDCI) Thiam aliondolewa, lakini ilikuwa ni matokeo ya kukosa kujiandaa kwa baadhi ya maafisa wa chama ndiko kulikosababisha aondolewe. Ndiyo maana unakuwa na silaha nyingi za kuchagua, hasa wakati unapokuwa kwenye siasa."

Tume ya uchaguzi ilichapisha orodha ya mwishi ya wagombea wiki iliopita, ila jina la Thiam halikuwepo, ambaye alieleza kughadhabishwa na uamuzi akiutaja kama "kutelekeza demokrasia".

Sheria ya Côte d'Ivoire inaeleza kuwa wagombea wote lazima wawe raia na hawatakiwi kuwa na uraia mwingine wowote.

Thiam aliukana uraia wake wa Ufaransa mwezi Februari ili aweze kutimiza vigezo vya kugombea kwenye uchaguzi.

Uraia wa Ufaransa wakati Thiam akisajili

Mahakama nchini Côte d'Ivoire ilihukumu mwezi Aprili kuwa Thiam aondolewe kwenye orodha ya uchaguzi kwa sababu alikuwa raia wa Ufaransa wakati akijisajili. Thiam aliliambia shirika la Reuters kuwa aliamua angeendelea kupambana na hadi kufikia kugombea.

Suala la uraia wa Côte d'Ivoire lilikuwa la msingi wakati wa machafuko ya siku za nyuma nchini Côte d'Ivoire, na wengine wanahofu kuwa suala la uraia wa Thiam kabla ya uchaguzi huenda likasababisha kurejea tena kwa hali ya vurugu.

Rais aliye madarakani Alassane Ouattara mwenyewe aliwahi kuzuiliwa kugombea urais kwa kile wapinzani wake walisema ni asili yake ya kigeni kabla kushinda uchaguzi 2010.

Ouattara, 83, hajasema kama atagombea tena mwaka huu.

Kuondoa vikwazo kuhusu uraia pacha

Billon ameiambia Reuters kuwa iwapo atachaguliwa ataidhinisha sheria ya kuondoa vikwazo kuhusu uraia pacha.

"Kuna maelfu ya raia wa Côte d'Ivoire ambao wanaishi nje ya nchi, ambao wamekuwa na makazi yao nje ya nchi, na wanakuwa na uraia pacha," alisema.

Billon pia amesema atapunguza wafanyakazi wa umma, kupambana na ufisadi, kuimarisha uwekezaji wa sekta binafsi na kuhamisha ofisi zaidi za serikali mjini Yamoussoukro, mji mkuu wa nchi.

Alisema ni wakati kwa Ouattara na wanasiasa wengine wa kizazi chake kuondoka madarakani.

"Côte d'Ivoire itabadilika. Nadhani wazee wetu wamekuwa na fursa yao," amesema.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us