UTURUKI
2 dk kusoma
Rais wa Uturuki aadhimisha Eid al Adha kwa ujumbe wa kuungana na Gaza, na maeneo mengine ya vita
Erdogan amesisitiza dhamira ya Uturuki ya kumaliza machafuko Palestina na kuhakikisha kuwa vita kati ya Urusi na Ukraine vinamalizika kukiwa na amani ya haki.
Rais wa Uturuki aadhimisha Eid al Adha kwa ujumbe wa kuungana na Gaza, na maeneo mengine ya vita
Erdogan ameeleza matumaini yake kuwa hali tete katika maeneo yenye mapigano, ikiwemo Gaza. Sudan na Somalia itakuwa sawa hivi karibuni. / AA
5 Juni 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa salamu za sikukuu ya Eid al Adha kwa Waislamu wote duniani, akitia wito wa kuungana pamoja na watu wa Palestina na jamii zingine zilizoathirika na mapigano.

"Kwa niaba ya nchi yangu na taifa langu, kwa heshima kabisa nawasalimu kaka na dada zetu wa Palestina ambao wanakabiliana na ukatili wa Israeli na ambao wanapambana kijasiri na matatizo huko Gaza na maeneo yaliyokaliwa," Erdogan alisema katika ujumbe kwa njia ya video siku ya Alhamisi.

Pia alituma salamu za rambirambi kwa wale waliopoteza maisha yao Gaza, akisema: “Tunawakumbuka kaka na dada zetu wote Gaza ambao wamekufa mashahidi katika mashambulizi haya kwa rehma, na nawaombea wale wote waliojeruhiwa wapate nafuu.”

Erdogan alieleza matumaini yake ya kuwa hali tete katika kanda mbalimbali iliyosababishwa na mapigano, ikiwemo Gaza, Sudan na Somalia itakuwa sawa hivi karibuni.

"Hatua ya kihistoria ya kumaliza vita vya kikatili”

Alisisitiza dhamira ya Uturuki ya kumaliza machafuko Palestina, akisema, “Tunafanya kila kilicho ndani ya uwezo wetu kusitisha mauaji ya halaiki Palestina na kuhakikisha kuwa vita kati ya Urusi na Ukraine vinamalizika kwa amani ya haki.”

Akiangazia juhudi za kidiplomasia, Erdogan alieleza kuhusu mkutano wa hivi karibuni jijini Istanbul 2 Juni, Jumatatu, akiueleza kama "hatua ya kihistoria ya kumaliza vita vya kikatili ambavyo vimeingia mwaka wake wa nne sasa."

Kuhusu majirani Syria, Erdogan amesema Uturuki imeridhishwa na juhudi za uongozi mpya wa nchi hiyo na kuunga mkono matumaini ya Syria yenye umoja wa kitaifa, uhuru wa mipaka yake, na maendeleo ya muda mrefu.

“Kwa kuungwa mkono na mataifa rafiki kwenye kanda yetu, tunaamini kuwa Syria itakuwa na amani ya kudumu na irudi kuwa kama zamani,” alisema.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us