AFRIKA
2 dk kusoma
Waislamu Kenya wachanga fedha kwa ajili ya Gaza
Chini ya mpango huo ng’ombe watanunuliwa na kuchinjwa nchini Misri, huku nyama iliyo katika barafu itasafirishwa hadi Gaza wakati njia za kupitisha misaada ya kibinadamu zitakapofunguliwa.
Waislamu Kenya wachanga fedha kwa ajili ya Gaza
Wakenya hao wameomba Bunge la Kenya kuweka swala la Gaza katika ajenda yake/ Picha: AA
5 Juni 2025

Jumuiya ya Waislamu nchini Kenya imechangisha kiasi cha fedha Ksh.5.4 milioni kulisha watu wa Gaza wenye njaa wakati wa Eid-ul-Adha kupitia Mpango wa Gaza-Udhiya 2025.

Mchango umeongozwa na Voice of Palestine. Huu ni muungano unaojumuisha Kamati ya Msikiti wa Jamia, Baraza Kuu la Waislamu wa Kenya, Jukwaa la Kitaifa la Viongozi wa Kiislamu, Baraza la Maimamu na Wahubiri wa Kenya, na wengineo.

"Tunasimama katika wakati mgumu ambapo ubinadamu unatuita kuchukua hatua. Watu wa Gaza, Palestina, wanastahimili mauaji ya halaiki na janga la kibinadamu ambalo halijawahi kushuhudiwa, linaloambatana na mateso na hasara kubwa," ilisema sehemu ya taarifa ya muungano huo.

Chini ya mpango huo ng’ombe watanunuliwa na kuchinjwa nchini Misri, huku nyama iliyo iliyopo kwenye barafu itasafirishwa hadi Gaza wakati njia za kupeleka misaada ya kibinadamu zitakapofunguliwa.

"Hii sio tu kuhusu kulisha wenye njaa-ni msimamo dhidi ya mauaji ya halaiki na ukosefu wa haki," alisema Ahmed Shariff, Mwenyekiti wa Voice of Palestine.

Muungano huo umetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja, kufunguliwa kwa njia za misaada, na msimamo thabiti wa kidiplomasia wa Kenya kuhusu mgogoro huo.

Viongozi walimtaka Rais William Ruto wa Kenya na Bunge la nchi hiyo kupaza sauti ya Kenya kwa ajili ya haki za binadamu.

"Tunatoa wito kwa Bunge la Kenya kutanguliza mgogoro huu kwenye ajenda yake," taarifa hiyo iliongeza.

Muungano huo ulitoa wito kwa Bunge la Kenya kujumuisha mgogoro wa Gaza katika ajenda yake na kuanzisha majadiliano kuhusu nafasi ya Kenya katika juhudi za kujenga amani.

Ulisisitiza umuhimu wa kutumia njia za kidiplomasia za Kenya kutetea amani na ulinzi wa haki za binadamu huko Gaza na eneo pana la Palestina.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us