Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, hii leo amelihutubia Baraza la Wawakilishi ambapo amezungumzia mambo kadhaa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 5 ya uongozi wake.
Rais Mwinyi, amesema kuwa katika mafanikio makubwa yaliyopatikana ni pamoja na kuimarika kwa uchumi, kuwepo kwa amani, na kuweza kuwaleta pamoja wananchi bila kujali itikadi zao za kidini na kisiasa.
Wakati huo huo, Rais Mwinyi, ametangaza kuwa atalivunja rasmi Baraza la Kumi la Wawakilishi ifikapo Agosti 13, 2025. Hatua hiyo ni kwa mujibu wa Kifungu cha 92 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Hichi ndio kitakuwa kikao cha mwisho cha Baraza la Wawakilishi kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Kwa mnasaba huo, Rais Mwinyi amewataka wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kushiriki katika uchaguzi.