AFRIKA
3 dk kusoma
Afrika Kusini yataka mabaki ya waliouawa enzi za ukoloni yarudishwe nyumbani
Afrika Kusini imedhamiria kuona mabaki ya waliouawa enzi za ukoloni na kupelekwa nje ya nchi pamoja na yale ya wanahaharakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi yamerejeshwa nyumbani.
Afrika Kusini yataka mabaki ya waliouawa enzi za ukoloni yarudishwe nyumbani
Afrika Kusini imeanza mchakato wa kutaka kurudishwa kwa mabaki ya raia wake waliokufa nje ya nchi wakati wa utawala wa kikoloni. / Picha: Reuters
9 Juni 2025

Afrika Kusini imedhamiria kuona mabaki ya waliouawa enzi za ukoloni ni kupelekwa nje ya nchi oamoja na yale ya wanahaharakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi yamerejeshwa nyumbani, waziri wa utamaduni alisema siku ya Jumatatu.

Serikali inawasiliana na taasisi za kigeni kuhusu kurejeshwa kwa mabaki ya watu wa asili ya Afrika Kusini, ikiwemo watu wa KhoiSan ambao wanaaminika kuwa miongoni mwa "watu wa kwanza" wa taifa hili, Waziri Gayton McKenzie amewaambia waandishi wa habari.

Wawakilishi wa serikali pia watatembelea nchi jirani za Angola na Zimbabwe kukagua kumbukumbu za makaburi kwa lengo la kuangalia kama kuna watu ambao huenda walizikwa huko wakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi ili waweze kurejeshwa, alisema.

"Haya ni masuala ya haki, kuwakumbuka watu na uponyaji," alisema. "Inabainisha dhamira ya serikali yetu kurudisha heshima,kuimarisha utamaduni, na kukabiliana na kumbukumbu mbaya ya ukoloni na ubaguzi wa rangi."

Kuwazika tena

Waziri wa michezo, sanaa na utamaduni ametangaza mpango wa kuzika tena mabaki ya watu wa asili 58 ambayo yalichukuliwa kwa ajili ya utafiti kwa makumbusho na taasisi zingine.

Baadhi ya mabaki hayo yalichukuliwa kutoka kwenye makaburi wakati wa utawala wa kikoloni, alisema.

"Yaliwekwa katika makumbusho, kufanyiwa utafiti katika maabara, na kuwekwa katika taasisi za kigeni bila idhini wala heshima. Tunarekebisha hali hii ya ukosefu wa haki," alisema.

"Tunatoa wito kwa taasisi zote, hapa nchini na nje ya nchi, kuanzisha mchakato wa haki na wenye matokeo wa kulipa fidia na kurejesha mabaki."

Familia hazikupata muda wa 'kuomboleza'

McKenzie ametaja kufanikiwa kuwarejeshwa mume na mke wa kundi la KhoiSan 2012, Klaas na Trooi Pienaar, ambao miili yao ilifufuliwa kinyume na sheria 1909 na kupelekwa Austria kwa ajili ya utafiti.

Pia akaeleza kuhusu kurejeshwa kwa mabaki ya mwanamke wa KhoiSan 2002, Sarah Baartman, aliyefariki dunia nchini Ufaransa 1815 baada ya kupelekwa Ulaya na kuwekwa kama kivutio cha nchi.

Baadaye, katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi uliomalizika 1994, "maelfu ya watu wetu walienda uhamishoni wakati wa mapambano hayo," McKenzie aliongeza.

"Wengi wao hawakurudi tena nyumbani. Wengine walikufa bila kutambuliwa, wakazikwa katika makaburi ambayo hayana majina yao, bila familia zao kupata nafasi ya kuomboleza," alisema.

Waliokufa wakiwa uhamishoni

Kuna wawakilishi wa serikali ambao watakwenda Angola katika wiki chache zijazo wakiwa na orodha ya watu 400 ambao wanawatafuta, amesema.

Serikali ilikuwa inafanya mazungumzo na shirika la Australia lenye uzoefu wa kutegua mabomu ya ardhini kuwasaidia kufika maeneo ya Angola ambayo bado yana mabomu ya ardhini miongo kadhaa tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe nchini Angola 2002.

Wanaharakati zaidi ya 1,000 wa kupinga ubaguzi wa rangi walikufa wakiwa uhamishoni maeneo mbalimbali barani Afrika lakini pia nchi ya Cuba na barani Ulaya, maafisa walisema mwezi Septemba wakati mabaki 42 ya waliokufa uhamishoni yaliporudishwa.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us