AFRIKA
1 dk kusoma
Kenya: Serikali yavifungia viatilifu 77 kwa sababu za kiusalama
Katika taarifa hiyo iliyotolewa Jumatatu Kagwe alisema kuwa hatua hiyo ilichochewa na hitaji la kukagua bidhaa vilivyosajiliwa kwa sasa katika soko la Kenya ili kuhakikisha kuwa Bidhaa zote za Kudhibiti Wadudu (PCPs) ni salama kwa afya ya binadamu na
Kenya: Serikali yavifungia viatilifu 77 kwa sababu za kiusalama
Kenya imepiga marufuku bidhaa zaidi ya 70 ya dawa za kuuwa wadudu/ Picha: Reuters
23 Juni 2025

Kenya imetangaza kuondoa kwenye mzunguko viatilifu 77, kwa sababu za kiusalama.

Katika taarifa yake ya Jumatatu, Waziri wa Kilimo nchini Kenya, Mutahi Kagwe amesema hatua hiyo inatokana na ukaguzi uliofanywa kwenye makundi yote ya madawa hayo ya kuulia wadudu.

“ Kwa hivyo, hii ilisababisha kuzuiwa kwa matumizi ya bidhaa 202 kwenye mazao mbalimbali, kwani bidhaa zingine 151 zimepitiwa na Bodi ya Kuthibiti dawa na sumu huku uamuzi ukifikiwa Disemba 2025,” ilisema taarifa hiyo.

Kati ya viatilifu vilivyopigwa marufuku ni pamoja na DDT ambayo ni dawa maarufu katika shughuli za kilimo, klorini pamoja na dawa ya kuondoa magugu.

Wizara hiyo, pia imeagiza usajili wa bidhaa zote za PCP kabla ya kuingizwa nchini Kenya.

Kulingana na wizara hiyo, PCP zilizopigwa marufuku kimataifa hazitosajiliwa kwa matumizi nchini Kenya na uagizaji wa molekuli yoyote inayokaguliwa ambayo haijaidhinishwa ndani ya Umoja wa Ulaya, Marekani, Australia, na Canada itapigwa marufuku hadi itakapokaguliwa.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us