ULIMWENGU
2 dk kusoma
Waziri wa ulinzi wa Israel anatishia kumega zaidi ardhi ya Palestine na kuitenga Gaza
Waasi wa Houthi wa Yemen washambulia uwanja wa ndege wa Ben Gurion, kituo cha kijeshi nchini Israel
Waziri wa ulinzi wa Israel anatishia kumega zaidi ardhi ya Palestine na kuitenga Gaza
Israel imeendeleza mauaji ya kimbari huku jeshi lake likiwaamuru raia wa Palestina walioko Khan Younis kukimbia / TRT World
14 Aprili 2025

Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz alitishia kunyakua zaidi ardhi ya Palestine na kuitenga Gaza huku mauaji yakiendelea katika eneo lililozingirwa.

"Gaza itakuwa ndogo na kutengwa zaidi, na wakazi wake wengi zaidi watalazimika kuhama kutoka maeneo ya mapigano," Katz alisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya X.

Huku hayo yakiripotiwa Waasi wa Houthi wa Yemen washambulia uwanja wa ndege wa Ben Gurion, kituo cha kijeshi nchini Israel Kundi la Houthi nchini Yemen lilidai kuhusika na mashambulizi matatu dhidi ya maeneo yanayolengwa na Israel.

Msemaji wa jeshi la Houthi Yahya Saree alisema kundi hilo lililenga uwanja wa ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv na kambi ya anga ya Sdot Micha katikati mwa Israel kwa makombora.

Marekani inatakiwa kufahamu zaidi - FIdan

Marekani inapaswa kufahamishwa vyema kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza - Fidan Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan alitoa wito kwa Marekani kufahamishwa vyema kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza na hatari za vita vinavyoendelea.

"Hadi sasa, kuendelea kwa mauaji ya halaiki ya sasa kumewezekana kupitia uungaji mkono wa Marekani, hasa kutokana na sera zilizoanzishwa wakati wa Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden.

Rais wa Marekani Donald Trump, wakati akiwa madarakani, alichangia kuanzishwa kwa usitishaji vita kupitia juhudi zake," Fidan alisema.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us