14 Aprili 2025
Mahakama nchini Japan, imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela raia wa nchi hiyo kwa kosa la kujeruhi na kuua sungura saba.
Riku Hotta, alihukumiwa siku ya Jumatatu kufuatia kosa hilo alilolitenda katika kisiwa cha Okuno kilichopo Hiroshima, eneo ambalo linajulikana pia kama ‘Kisiwa cha Sungura’.
Mahakama ya Wilaya ya Hiroshima ilimkuta Hotta na hatia ya kuua sungura wapatao saba, huku Jaji Wataru Shimazaki akikiita kuwa ni kitendo “kiovu”.
Hotta alikamatwa mwezi Januari baada ya kupatikana akimpiga sungura teke katika kisiwa hicho.
Mnyama huyo aliripotiwa kufa kutokana na majeraha aliyoyapata.
Kufuatia tukio hilo, Wizara ya Mazingira nchini Japan imepanga kufunga kamera za siri ndani ya kisiwa hicho ili kubaini matukio mengine kama hayo.