Changamoto za mzazi wa kiume au maarufu "single fatherhood"
Changamoto za mzazi wa kiume au maarufu "single fatherhood"
Baba asiye na mke au mwenza anaweza kuwa na wasiwasi ikiwa anaweza kumtunza mtoto wake vizuri na kunaweza kuwa na maeneo ambapo anahisi upungufu wa kibinafsi na anahitaji msaada kutoka kwa wengine.
18 Julai 2025

Familia zinabadilika kote ulimwenguni na familia za mzazi mmoja zinazidi kuwa za kawaida katika nchi nyingi, hasa kutokana na kuongezeka kwa viwango vya talaka na wanandoa kupata watoto nje ya ndoa.

Mara nyingi utakuta familia hizi huwa za mama pekee, lakini katika miaka ya hivi karibuni, kina baba wengi wamejitolea kulea watoto wao wakiwa peke yao. Kina baba mara nyingi huenziwa kwa furaha na muunganisho wake, lakini kwa kina baba wasio na wenza, jukumu hili linakuwa na changamoto za kipekee ambazo mara nyingi hazichukuliwi kwa uzito.

Katika jamii zetu, hasa za Kiafrika, jamii, familia, na tamaduni zina matarajio tofauti inapokuja kwa majukumu ya kijinsia na kama inafaa kwa mwanamume kuchukua jukumu la mlezi mkuu katika familia. Changamoto hii ni kukabiliwa na unyanyapaa kutoka kwa jamii kwa mtazamo wa jamii au fikra potofu. Mitazamo fulani inaweza kufanya iwe vigumu kwa baba wa watoto kupata usaidizi unaohitajika wakati wa shida.

Baba asiye na mke au mwenza anaweza kuwa na wasiwasi ikiwa anaweza kumtunza mtoto wake vizuri na kunaweza kuwa na maeneo ambapo anahisi upungufu wa kibinafsi na anahitaji msaada kutoka kwa wengine.

Kwa Bashir Idris Abubakar kutoka Nigeria, alijikuta katika hali ya kuwa mzazi pekee baada ya msiba. Alifunga ndoa na mkewe mwisho wa mwaka wa 2020 na kujaaliwa mtoto wa kike mwisho wa mwaka wa 2021. Baada ya miaka miwili, Bashir alipata kazi nje ya nchi na akasafiri na kumuacha mkewe akiwa mjamzito na mtoto wa pili.

Alipokuwa huko, mkewe aliugua na akaaga dunia. Kwa Bashir, hili lilimvunja moyo sana kwani alikuwa ameazimia kujenga maisha yake na mkewe na watoto wao. Changamoto ya kwanza kwake ni kuzowea maisha bila mkewe, jambo ambalo bado anapambana nalo.

Bashir ilibidi amuache mwanawe Nigeria alelewe na familia yake. Ijapokuwa anashukuru kupata usaidizi kutoka kwa familia yake kumsaidia kumlea mwanawe anahisi kuwa yeye kama baba hapati nafasi ya kuwa katika maisha ya mwanawe na kuweza kumlea anavyohisi kuwa ndiyo malezi anayotaka mwanawe awe nayo. Hii ni changamoto inayowakumba kina baba wengi ya kuweka mizanina ya majukumu ya kazi na ulezi.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us