Wataalamu wa magonjwa katika Kliniki ya Cleveland wanasema ugonjwa wa CVI unasababishwa na upungufu wa muda mrefu wa venous (CVI) ambao hutokea wakati mishipa yako ya mguu inaharibiwa na haiwezi kufanya kazi inavyopaswa.
Kliniki ya Cleveland ni kituo cha matibabu cha kitaaluma cha Marekani kisicho na faida kilichoko Cleveland, Marekani.
Kwa kawaida, vali kwenye mishipa ya mguu wako huweka damu inapita hadi moyoni mwako.
Lakini CVI huharibu vali hizo, na kusababisha damu kukusanyika kwenye miguu yako. Hii huongeza shinikizo kwenye mishipa ya mguu wako na husababisha dalili kama vile uvimbe na vidonda.
Ikiwa una CVI, vali kwenye mishipa yako (kwa kawaida kwenye mguu au wakati mwingine mikono), hivyo kusababisha damu kukusanyika kwenye miguu yako na kuongeza shinikizo kwenye kuta za mishipa.
Dalili kuwa una CVI
Kulingana na Kliniki ya Cleveland huenda usiwe na dalili zote za ugonjwa huu kwa wakati mmoja.
Badala yake, unaweza kuwa na dalili moja au mbili tu. Ishara na dalili zako hutegemea jinsi hali yako ilivyoendelea.
Miguu inayouma au ina uchovu.
Kuungua, kupiga au "pini na sindano" hisia kwenye miguu yako.
Kuvimba kwa miguu usiku.
Ngozi iliyobadilika rangi inayoonekana nyekundu-kahawia.
Uvimbe kwenye miguu yako ya chini na vifundoni, haswa baada ya kusimama kwa muda au mwisho wa siku.
Kuvimba au kuwasha kwa ngozi kwenye miguu
Hisia nzito katika miguu yako.
Vidonda wazi kwa kawaida karibu na vifundo vyako.
Ushauri wa wataalamu wa kukabiliana na ugonjwa wa CVI
Kuinua miguu
Kuinua miguu yako juu ya kiwango cha moyo wako kunaweza kusaidia kupunguza shinikizo kwenye mishipa yako ya mguu. Mtoa huduma wako anaweza kupendekeza ufanye hivi kwa dakika 30 au zaidi angalau mara tatu kwa siku.
Fanya zoezi
Kutembea na aina nyengine za mazoezi zinaweza kusaidia damu kutiririka vyema kwenye mishipa yako ya mguu. Kila wakati unapopiga hatua, misuli ya chini ya miguu yako inabana na kusaidia mishipa yako kusukuma damu hadi kwenye moyo wako.
Kudhibiti uzito wako
Uzito wa ziada unaweza kuweka shinikizo kwenye mishipa yako na kuharibu vali. Unafaa kumuuliza mtaalamu wa afya ni uzito gani unaofaa kuwa nao. Fanya kazi na mtoa huduma wako ili kupata mpango mzuri na unaoweza kudhibitiwa wa kufikia uzito huo.
Matibabu ya CVI
CVI kawaida haihatarishi maisha na haisababishi kukatwa kwa miguu.
Lakini ni ugonjwa ambao unaweza kusababisha usumbufu, maumivu na kupunguza ubora wa maisha.
Matibabu yanaweza kusaidia kudhibiti dalili zako na kukupa maisha bora.
Vidonda vya miguu ni vigumu kutibu, na vinaweza kurudi hata baada ya matibabu.