AFRIKA
1 dk kusoma
Mpox bado ni ugonjwa wa dharura: WHO
Mlipuko wa ugonjwa wa mpox bado ni tatizo la kiafya la dharura, Shirika la Afya Duniani WHO limesema siku ya Jumatatu.
Mpox bado ni ugonjwa wa dharura: WHO
Juhudi za chanjo dhidi ya mpox zinaendelea barani Afrika. / Picha: Reuters
9 Juni 2025

Mlipuko wa ugonjwa wa mpox bado ni tatizo la dharura la kiafya, Shirika la Afya Duniani lilisema Jumatatu, huku Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo akitoa utaratibu mpya pamoja na mapendekezo ya muda ya kufuatwa.

Mara ya kwanza kwa WHO kutangaza ugonjwa huo kuwa dharura ilikuwa mwezi Agosti mwaka uliopita, wakati mlipuko wa aina tofauti ya mpox ulipoibuka na kuenea kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hadi katika mataifa jirani.

Kutangaza hali ya dharura kwa afya ya umma kimataifa ni onyo la hali ya juu la tahadhari kutolewa na WHO.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us